1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania, Italia zatinga 16 bora

Admin.WagnerD18 Juni 2016

Alvaro Morato aliwafungia mara mbili mabingwa watetezi Uhispania na Eder alikuwa mshindi wa Italia wakati timu hizo mbili zikikata tiketi ya 16 bora ya michuano ya Euro2016 katika siku nyingine iliyogubikwa na vurugu.

https://p.dw.com/p/1J96q
Mabingwa watetezi Uhispania wakati wa mechi dhidi ya Uturuki.
Mabingwa watetezi Uhispania wakati wa mechi dhidi ya Uturuki.Picha: Reuters/Y. Herman

Mchezo uliomalizika kwa Sare ya 2-2 kati ya Croatia na Jamhuri ya Czech ulisimamishwa kwa muda baada ya Wacroatia kurusha mieko uwanjani, na kumlaazimu Kocha Ante Cacic kuwaita "magaidi ya michezo."

Shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA limeahidi kuchunguza, na Uturuki pia inaweza kukabiliwa na adhabu ya shirikisho hilo baada ya mashabiki wake kurusha fataki uwanjani mwishoni mwa mechi yao walioshindwa 3-0 na Uhispania.

Uwanjani lakini, Uhispania imesistiza dhamira yake ya kuwa timu ya kwanza kushinda ubingwa wa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo. Vijana hao wa Vicente del Bosque wamekuwa wa kwanza kushinda magoli matatu katika siku ya nane ya mashindano hayo yanayofanyika Ufaransa.

Mchezaji wa Jamhuri ya Czech Tomas Necid akifunga goli dhidi ya Croatia katika uwanja wa Saint-Etienne. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
Mchezaji wa Jamhuri ya Czech Tomas Necid akifunga goli dhidi ya Croatia katika uwanja wa Saint-Etienne. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.Picha: Reuters/J. Cairnduff

Mshambulijai wa Juventus Morata alifunga mara mbili na kuendeleza kasi ya Uhispania baada ya Gerard Pique kufunga goli la dakika za mwisho dhidi ya Jamhuri ya Czech katika mechi yao ya ufunguzi.

Pamoja na hayo, alikuwa mchezaji wa kati wa Barcelona Andre Iniesta alieibuka na tuzo ya mchezaji bora wa mechi. Uhispania sasa inaweza kuchukuwa nafasi ya kwanza ya kundi lake kwa sare dhidi ya Croatia katika mechi yao ya mwisho ya kundi siku ya Jumanne.

Uturuki yahitaji miujiza

Uturuki sasa itahitaji kushinda dhidi ya Jamhuri ya Czech katika mechi yao ya mwisho ya makundu na iombe matokeo mengine yaende upande wake ili kuw ana nafasi ya kusonga mbele kama moja ya timu nne bora zilizoshika nafasi ya tatu kutoka makundi sita.

Italia ilijipatia nafasi ya kucheza duru ya mtoano katika mechi iliyochezwa kwa utulivu mjini Toulouse wakati mshambuliaji mzaliwa wa Brazil Eder alipofunga goli lenye ustadi mkubwa dakika mbili kabla ya firimbi ya mwisho na kuhitimisha ushindi wa moja bila dhidi ya Sweden ya mchezaji Zlatan Ibrahimovich.

Baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland siku ya Jumatano, Sweden sasa inakabiliwa na hatari ya kufungashiwa virago ikiwa watashindwa kuifunga Ubelgji katika mechi yao ya mwisho ya makundi.

Mfungaji wa goli pekee la Italia Eder akishangilia baada ya kuifunga Sweden.
Mfungaji wa goli pekee la Italia Eder akishangilia baada ya kuifunga Sweden.Picha: Reuters/M. Dalder

Ibrahimovic alikosa tena fursa ya kuwa wa mtu wa kwanza kufunga goli katika mashindano matatu mfululizo ya bingwa wa Ulaya. Mchezaji huyo anaelengwa na Mancgester United alisema katika mechi ya kwanza hawakufanya chochote lakini walipata point moja, lakini katika mechi ya Ijumaa ambayo wamefanya kazi nzuri wametoka patupu.

Wakati huo huo, kocha wa Uturuki Fatih Terim amewakripia mashabiki wa nchi hiyo kw akumzomea mchezaji nyota Arda Turan wakati timu yake ikipigwa 3-0 na Uhispania.

Terim amewambia wandishi wa habari mjini Nice baada ya mechi hiyo ya kundi D kwamba licha ya kuwa mashambiki walikuw ana matumaini makubwa, lakini anaepaswa kuzomewa.

Mwandishi: Iddi Ssessanga

Mhariri: Mohammed Khelef