1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhuru wa Kosovo ?

23 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CfPM

KOSOVO:

Mawaziri wa nje wa Ugiriki,Romania na Bulgaria wameitisha mazungumzo zaidi juu ya hatima ya mkoa wa Kosovo unaotaka kujitenga na Serbia na kuwa nchi huru.

Mawaziri 3 hao wasliokutana mjini Athens jana walisisitiza halkadhalika kwamba mustakbala wa Serbia uko ndani ya Umoja wa Ulaya na kuwa kujiunga na umoja huo siku zijazo kusifungamanishwe na matokeo ya Kosovo.

Majadiliano juu ya hatima ya Kosovo yalivunjika mapema mwezi huu baada ya Baraza la Usalama la UM lilishindwa kuafikiana.

Wingi wa nchi za Ulaya pamoja na Marekani unaungamkono Kosovo kuwa nchi huru.Russia lakini inaungamkono msimamo wa Serbia kuwa jimbo la Kosovo lisalie chini ya mamlaka ya Serbia.90% ya wakaazi wa Kosovo ni waalbania.