1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yakiri kulikuwepo safari za siri za CIA

22 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DBS6

LONDON:

Uingereza imekiri kuwa ndege za Marekani zilitumia ardhi yake kuwasafirisha kwa siri washukiwa ugaidi waliotekwa nyara.Hapo awali serikali ya Uingereza ilikanusha kabisa kuhusu safari hizo zilizohusika na operesheni za Shirika la Ujasusi la Marekani CIA.Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Miliband ameliambia bunge mjini London,habari mpya zimepatikana baada ya Marekani kuchunguza upya rekodi zake.

Kwa mujibu wa habari hizo mpya,ndege hizo katika mwaka 2002,zilitua kisiwani Diego Garcia kujaza mafuta kama mara mbili.Kisiwa hicho katika Bahari ya Hindi kipo chini ya utawala wa Uingereza.Ikulu ya Marekani imesema,shirika la CIA lilifanya makosa liliposhindwa kuiarifu Uingereza.Safari hizo zilianza baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001