1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani bingwa wa dunia-miundo-mbinu

24 Septemba 2010

Uchumi ukikua,biashara hii yazidi kustawi.

https://p.dw.com/p/PLe1
Ujerumani yapepea bendera ya (miundo-mbinu)Picha: picture alliance/dpa

Ujerumani, ni mabingwa wa dunia kwa mipango ya miundo-mbinu. Hivyo ndivyo, usemavyo uchunguzi mpya unaotolewa kila baada ya miaka 2 wa Banki kuu ya Dunia kuhusu kile kinachoitwa "Muongozo wa mipango ya miundo-mbinu (LPI) kwa ufupi.

Miongoni mwa mataifa 155 duniani, Ujerumani imetawazwa mabingwa wa dunia katika mipango ya miundo-mbinu, kama kuongoza mawasiliano na uchukuzi hata usafiri wa bidhaa na shehena.

Tawi hili la mipango ya miundombinu ambalo ndilo kwanza linafufuka kutoka msukosuko wa kiuchumi, ndipo Ujerumani iliposhika usukani ulimwenguni. Mwaka jana, 2009, biashara ulimwenguni ilianguka kwa kima cha 12% na kwa nchi kama Ujerumani hii ina maana:

Viwanda kama vile vya meli zinazosafirisha shehena kwa njia ya bahari, makampuni yanayosafirisha shehena -cargo- kwa ndege hewani, misafara ya meli zinazosafirisha bidhaa kupitia mito ya ndani ya nchi pamoja na ile ya barabarani ya malori ilipungua kwa kima cha 11 %. Pato jumla kutokana na shughuli hizo za biashara ya miundo-mbinu na usafiri kwa mwaka uliopita lilikuwa Euro Bilioni 200 nchini Ujerumani, kama 2007 kabla kuzuka msukosuko.

Kwa hali hii, viwanda vya mipango na miundo-mbinu vinabakia kuwa tawi linaloongoza kabisa kiuchumi Ujerumani.

Na kwa vile uchumi umeaanza kukua tena, matumaini yamerudi kustawi tena kwa tawi hili.Kwa hivyo, gurudumu la viwanda vya mipango ya miundo-mbinu limerudi kuzunguka kwa kasi tena nchini Ujerumani mwaka huu 2010 .

Viwanda hivi vimeongeza usafirishaji wa bidhaa na shehena kwa kima cha 7% na zaidi tangu kwenye barabara kuu hata baharini. Upande wa reli, misafara imeongezeka kwa 11% kuliko ilivyokuwa mwaka uliopita wa msukosuko wa uchumi. Muongezeko wa 19% umepatikana katika misafara ya shehena za ndege-cargo, hivyo ndivyo wizara ya usafiri na uchukuzi ya Ujerumani, ilivyobashiri kwa mwaka huu wa 2010.

Mwaka jana tu, sura ya mambo ilikuwa vyengine kabisa. Safari za magari-moshi inayopakia shehena zilisimama ,meli zinazopakia makontena hazikuwa na safari tena na misafara ya shehena za ndege zilisimama kabisa.

Bada ya kukua biashara hizi kwa kima cha 9%, biashara ya mipango ya miundo-mbinu iliporomoka kabisa. Hata shirika la ndege la LUFTHANSA , linalopakia mizigo liliathirika mno. Mnamo muda mfupi, sio tu mtandao mzima wa misafara ya cargo uliyumbayumba -anasema Bw. Andreas Jahnke, Kiongozi wa shughuli za mipango na miundo-mbinu wa kampuni la ndege la LUFTHANSA:

"Kwa jumla, jambo lisilofurahisha kabisa wakati wa msukosuko huu, ni kurundikana mno kwa shehena zilizohitaji kusafirishwa hali ilioongoza kuteremka bei."

Kwa hivyo, baada ya dhiki si dhiki : Kupambazuka haraka kwa tawi hili la miundo-mbinu, uchukuzi na misafara, na hasa zile za anga na za baharini, kwa jicho la mishahara ya juu inayolipwa Ujerumani, yamkini, kumewasangaza baadhi ya watu nchini Ujerumani.

Mwandishi:Fuchs,Richard/ZRP Tayarishi: Ramadhan Ali Uhariri :

Miraji Othman