1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani imeitambua Kosovo

Miraji Othman20 Februari 2008

Tunakumbuka miaka 17 iliopita? Ujerumani ilikuwa nchi ya kwakwa kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Kroatia, Slovenia na Macedonia.

https://p.dw.com/p/DAaT
Martti Ahtissari, rais wa zamani wa Finnland na mtu aliyetunga mpango wa kuipatia Kosovo uhuruPicha: AP

Kutokana na uamuzi wa jana, serekali ya Ujerumani inauchukulia sasa ule ukweli kwamba kusambaratika kwa uchungu Yogoslavia ya zamani sasa kumefikia ukomo wake, zoezi ililloanza miaka 20 iliopita, na lililoanzia Kosovo.

Kutambuliwa Kosovo kama nchi ni ushahidi juu ya nia ya Ujerumani ya kuongoza pamoja na nchi zote zilizochokuwa kwa pamoja hatua hiyo mnamo siku chache zilizopita na pia zile nchi zinazoendelea kuchukuwa hatua hiyo. Lakini sasa kinachotakiwa hasa ni kuthibitisha juu ya nguvu hiyo ya kuongoza, tena kuiimarisha kwa vitendo. Ujerumani, pamoja na nchi za Ummoja wa Ulaya zilizotuma ujumbe wa kuanzisha mifumo ya utawala wa sheria huko Kosovo, lakini pia na Marekani, zinafaa zidhihirishe kuweko kwao kijeshi katika nchi hiyo ya Balkan. Jambo hilo ni muhimu kwa nchi hiyo mpya kupata mafanikio.

Itazamiwe kwamba wapinzani wa uhuru wa Kosovo, mbele kabisa zikiwa serekali za Serbia na Russia, zitafanya kila zinavoweza kudhihirisha kwamba Kosovo inashindwa kama dola. Michafuko iliotokea katika mpaka wa Kosovo hapo juzi, jumanne, imeshatupa sura ya hali ya mambo itakavoweza kuwa.Waziri wa Serbia anayeshughulikia masuala ya Kosovo, Slobodan Samardzic, ameikaribisha na kuielezea michafuko hiyo kuwa ya halali.Pia Serbia inawabinya sana watu wenye asili ya Ki-Serbia ambao wanafanya kazi katika jeshi la polisi la Kosovo, waache kazi.

Kitu kilicho kibaya kabisa ambacho watu wenye asili ya Ki-serbia wanaweza kufanya ni kujitoa kutoka taasisi za serekali ya Kosovo. Ujerumani na nchi zote zilizoitambua Kosovo lazima sasa, pamoja na serekali ya Kosovo, ziwashawishi Wa-Serbia wasifanye hivyo. Lazima waweke wazi kwa Wa-Serbia wa Kosovo kwamba taasisi za serekali ya nchi hiyo zinaweza kuwapa usalama na mustakbali mzuri zaidi kuliko watawala wa Serbia ambao, kwa sababu tu za kisiasa, wanajaribu kuubakisha mzozo huo uwe moto.

Na ili kuwapa Wa-Serbia hao usalama na mustakbali, wabunge wa Kosovo punde hivi wamepitisha sheria za uanze kufanya kazi mpango wa Martti Ahtisaari, yule mwakilihsi wa Umoja wa Mataifa aliyependekeza juu ya mustakbali wa Kosovo kuwa nchi huru, lakini bado chini ya ulinzi wa Umoja wa Ulaya. Mpango huo unayahakikishia makabila ya wachache haki nyingi. Sasa inahitaji haki hizo zijazwe na kuboresha maisha ya watu, hivyo kuzuwia kujitenga kwa Wa-Serbia walio wachache huko Kaskazini mwa Kosovo na kutangazia nchi yao.

Hali hiyo inawezekana tu ikiwa taasisi za serekali huko Kosovo na pia jeshi la kulinda amani la kimataifa zitabaki zina mamlaka na bila ya kuchelea kupinga kuweko taasisi zozote zinazotaka kuendesha mambo sambamba na ambazo Serbia itajaribu kuzianzisha. Pindi jaraibi hilo litafanywa na Serbia, basi hali hiyo itarefusha tu shida za Wa-Serbia wa Kosovo na kuzuwia kujichanganyisha katika jamii ya Kosovo.

Ili kuzuwia machungu kama hayo, ni pia muhimu kwa Serbia ijifungamanishe na Umoja wa Ulaya. Ni tu pale siasa za Serbia zitakapoachana na ndoto za kuweza kuitawala Kosovo, ndipo nchi hiyo itakapoachana na mambo yaliopita na itakapoweza kuendeleza fikra ya kuuweka mustakbali wake pamoja na Umoja wa Ulaya.