1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani inasafiri hadi Azerbaijan

6 Juni 2011

Timu ya taifa ya Ujerumani inakaribishwa na Azerbaijan kwenye mpambano wa kirafiki siku ya Jumanne

https://p.dw.com/p/11VMN
Timu ya taifa ya Ujerumani inatafuta Ushindi mwinginePicha: dapd

Timu ya taifa ya Ujerumani ambayo haijashindwa mpaka sasa katika mipambano 6 ya kirafiki inatafuta ushindi wa saba mtawalia katika kufuzu kwenye mashindano ya Euro 2012 inapotarajiwa kukutana na wenyeji Azerbaijan hapo kesho huku mpambano huo pia huenda ukatoa hatima ya mkufunzi wa Azerbaijan,Berti Vogts.

Deutschland gegen Uruguay 2011
Nambari 23 mgogongoni, Mario GomezPicha: picture alliance/dpa

Ujerumani imewaita wachezaji wake Lewis Holtby na Sebastian Rudy hapo jana kuziba pengo la wachezaji walio nje kutokana na maumivu kwenye timu hiyo inayoongoza katika kundi A, na yenye pointi 18 mpaka sasa kutoka michezo yake sita ukiwemo ushindi wao wa mabao 2-1 siku ya Ijumaa dhidi ya Austria.

Loewe anawakosa kwenye kikosi chake wachezaji muhimu kama vile Bastiana Schweinsteiger na Sami Khedira,matumaini yake yote sasa yapo kwa mshambuliaji wa pekee Mario Gomez ambaye huenda akaongeza hesabu ya mabao yake 45 yakijumuisha ya klabu na ya kitaifa katika mashindano yote msimu uliopita. Aliifungia Ujerumani mawili dhidi ya Austria siku ya Ijumaa.

Joachim Löw
Kocha Joachim Loewe.Picha: dapd

Loewe amesema kuwa ana matumaini kuwa kikosi chake kitawajibika vilivyo Azerbaijan maana sio kazi rahisi kutokana na kuwa hata Uturuki ilifungwa huko.

Baada ya Ujerumani, timu ya taifa ya Ubelgiji ni ya pili kwenye kundi hilo A, ikiwa na pointi 11 kwenye michezo 7 na Uturuki ikiwa namabari 3 kwa pointi 10 kutokana na mechi 6. Azerbaijan ipo katika nafasi ya mwisho sawa na Kazakhstan zikiwa na pointi 3 kila mmoja.

Ama kwa upande wa Mjerumani mwenzake kocha Berti Vogts, matatizo anayo lna yenye uzito mkubwa zaidi. Kichwa kinamzunguka kocha huyo wa Azerbaijan, kufuatia mechi ya hapo kesho dhidi ya Ujerumani, baada ya kuvamiwa na wanaume watatu katika mkutano na waandishi habari hapo jana kufuatia kufungwa timu yake na ile ya kazakhstan siku ya Ijumaa.

Hatahivyo Vogts ambaye amewahi kuifunza timu ya taifa ya Ujerumani na kuiongoza kuchukua taji hilo la Ulaya mnamo mwaka 1996, na aliyeshinda kombe la dunia la mwaka 1974 alipoichezea timu ya taifa nchini humo, aliponea chupuchupu baada ya maafisa wa usalama kumuokoa dhidi ya vikombe vya kahawa na makaratasi aliyorushiwa.

Berti Vogts Nationaltrainer Aserbaidschan
Kocha Berti Vogts, kulia, wa AzerbaijanPicha: AP

Vogts aliyepigwa na mshtuko alisema kuwa angekuwa tayari ameshajiuzulu wadhifa wake iwapo sio kwa urafiki alio nao na rais wa shirikisho, aliongeza kuwa ameshawahi kupitia mengi lakini sio tukio kama la jana kiasi cha kukosa maneno ya kuelelieleza tukio hilo.

Duru katika vyombo vya habari zinasema huenda Vogts akahamia katika timu ya Uturuki, iwapo Guus Hiddink ataelekea kuifunza timu iliopo kwenye ligi ya Uingereza, Chelsea.

Ama katika taarifa za uhamisho na usajili wa wachezaji katika ligi ya Ujerumani Bundesliga, hivi leo Mfungaji mkongwe nchini Ujerumani Miroslav Klose anaihama timu ya Bayern Munich mwishoni mwa mwezi huu.

Klose anayetimiza miaka 33 siku ya Alhamisi, anatarjiwa kuihama Bayern kufuatia kukamilika kandarasi yake na timu hiyo mwishoni mwa mwezi huu na duru zinasema kuwa huenda akatangaza mabadiliko katika uchezaji wake kutoka ligi ya Ujerumani na kuingia katika ligi ya Uhispania.

Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani Der Bild, mchezaji huyo nyota aliyefunga mabao 61 katika mechi 109 za kamataifa amekataa ombi la Bayern la kumuongezea muda wa kuhudumu katika timu hiyo ya Bavaia kwa mwaka mmoja zaidi.

WM 2010 - Deutschland Pressekonferenz
Mchezaji Miroslav KlosePicha: picture-alliance/dpa

Gazeti hilo linaripoti kuwa Klose alitaka kuongezewa miaka miwili na mshahara mkubwa zaidi ya Bayern inavyoweza kuumpa.

Klose amekuwa kwenye timu ya Bayern tangu mwaka 2007 na timu nyingi ikiwemo ya Italia Lazio na Everton ya Uingereza zinasemekana kumwania.

Katika miaka minne Klose amefunga mabao 53, katika michezo 150 na Bayern na anaikaribia rekodi ya Gerd Mueller ya kuifungia Ujerumani mabao 68.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Afpe/Rtre/Dpae
Mhariri: Abdul-Rahman.