1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani ipeleke majeshi kusini mwa Afghanistan

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1aU

BERLIN:

Licha ya upinzani wake,serikali ya Ujerumani inashinikizwa na Shirika la Kujihami la Magharibi NATO kuongeza shughuli zake za kijeshi nchini Afghanistan.Katibu Mkuu wa NATO,de Hoop Scheffer amesema,majeshi ya Ujerumani yasiwekwe kaskazini mwa Afghanistan tu.Sawa na Marekani,Kanada pia inadai kuwa wanajeshi wa Ujerumani vile vile wapelekwe katika eneo la mapigano,kusini mwa Afghanistan.

Ujerumani ina takriban wanajeshi 3,200 kaskazini mwa Afghanistan kama sehemu ya vikosi vya NATO.Wanajeshi wa Ujerumani katika eneo hilo la usalama fulani, hasa wanashughulikia miradi ya kuijenga upya Afghanistan.