1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuchuana na Ureno leo

Tsuma, Carolyne16 Juni 2014

Ujerumani leo jioni (16.06.2014) itamenyana na Ureno katika mechi za kundi G za mashindano ya kombe la kandanda la dunia yanayoendelea nchini Brazil.

https://p.dw.com/p/1CJ9Y
Fußball WM 2014 Nationalmannschaft Deutschland Training 14.6.2014
Picha: REUTERS

Kocha wa Ujerumani Joachim Loew amesema itakuwa vigumu kuilaza timu yake iwapo wachezaji wake watatumia uwezo wao. Kwa upande wa Ureno pia watakuwa wanategemea pakubwa mchango wa mchezaji wao nyota Christiano Ronaldo kuibuka na ushindi katika mechi hiyo ya makundi. Marekani nayo itachuana na Ghana leo usiku katika mechi ya kundi G. Timu nyingine ya Afrika- Nigeria itakuwa uwanjani dhidi ya Iran katika ya kundi F.