1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaadhimisha miaka 25 ya muungano

3 Oktoba 2015

Leo (03.10.2015) Ujerumani inaadhimisha miaka 25 tangu kuungana, Ujerumani ya mashariki na ile ya magharibi. Miaka 25 baada ya muungano, Ujerumani hata hivyo bado haina hakika ya nafasi yake duniani.

https://p.dw.com/p/1Gi1Y
Tag der Deutschen Einheit Peter Feldmann Joachim Gauck Angela Merkel Ursula Bouffier Volker Bouffier
Picha: Reuters/K.Pfaffenbach

Viongozi wa kisiasa mjini Berlin wanajitenga na maneno kama "nguvu ya dunia" lakini nchi hiyo italazimika kupambana na matokeo ya jukumu kubwa inalotakiwa kuchukua wakati Ujerumani ikichukua majukumu ya kimataifa.

Katika siku ambayo nchi mbili za Ujerumani ziliungana miaka 25 iliyopita , kansela wa wakati huo , Helmut Kohl, alituma ujumbe kwa dunia nzima, kwamba "ni amani tu itakayotoka katika ardhi ya Ujerumani katika siku za baadaye."

Joachim Gauck Tag der Deutschen Einheit Frankfurt Straßenszene Bürger
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck akiwasili mjini Frankfurt kuadhimisha Siku Kuu ya MuunganoPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

"Tunafahamu kwamba kwa muungano huu tumechukua jukumu kubwa katika jamii ya kimataifa kwa jumla," amesema Kolh katika barua yake ya oktoba 3, 1990, iliyotumwa kwa nchi zote ambazo Ujerumani inamahusiano nayo ya kidiplomasia.

Jukumu la Ujerumani kwa dunia

Wakati maadhimisho ya leo Jumamosi (03.10.2015)yanapita kwa kiasi kikubwa bila ya matukio makubwa, mtazamo duniani kote umelenga katika jukumu la Ujerumani kwa deni la Ugiriki, mzozo wa Ukraine na hivi sasa wimbi la wakimbizi wanaoingia barani Ulaya.

Kwa kuwa na uchumi mkubwa barani Ulaya na hivi sasa ikiwa ni nchi yenye nguvu za kisiasa, Ujerumani inachukua nafasi ya udhibiti katika Umoja wa Ulaya.

Ushiriki wa kisiasa wa Ujerumani ni sababu nyingine. Angela Merkel, baada ya miaka 10 madarakani kama kansela, anaonekana kwa kiasi kikubwa kama mwanamke mwenye nguvu nyingi katika bara la Ulaya. Jarida la Forbes limemchagua kuwa mwanamke mwenye nguvu nyingi za madaraka duniani.

Berliner Mauerstück in Washington
Sehemu ya ukuta wa BerlinPicha: picture-alliance/dpa/Peter Endig

Na baada ya miaka yake mingi kama waziri wa mambo ya kigeni, Frank-Walter Steinmeier pia ana nafasi yake katika ulimwengu wa kisiasa.

Wakati ikikubalika kwamba Ujerumani inapaswa kuridhia kuchukua jukumu kubwa zaidi, Berlin hata hivyo inachukua kwa tahadhari mno suala la iwapo ni mji mkuu wa madaraka ya kikanda, madaraka makubwa ama madaraka ama nguvu ya dunia.

Kwa kawaida kinachojitokeza mara nyingi ni tabasamu lisilokuwa na uhakika.

Washirika ni muhimu kwa Ujerumani

Akiulizwa maoni yake hivi karibuni , Merkel amesema : "Situmii maneno hayo. Sijawahi kutumia maneno, "nguvu ya kati" ama "nguvu ya dunia"wakati wowote ule."

Ameongeza: "Kile ambacho ni sahihi ni kwamba ukweli kwamba tumepata nchi yetu kamili kupitia muungano wa Ujerumani kuna matokeo yake kwa mtazamo mzuri, lakini pia kwa kuangalia kuchukua majukumu - na hii si zaidi wala pungufu."

Amemaliazia: "Na bila washirika hatuwezi kufanikiwa lolote." Hii inaakisi maelezo kwamba Ujerumani haingekuwa na ushawishi mkubwa bila kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya na NATO katika enzi ya utandawazi, pamoja na mtazamo kwamba ni kwa maslahi makubwa ya Ujerumani ikipuuzia umuhimu wake - la sivyo mara moja itatengwa na kurefushwa.

Kwa sasa lakini kila mmoja anaiangalia Ujerumani kwa uongozi.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Issac Gamba