1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaanza kampeni ya EURO 2016

5 Septemba 2014

Ujerumani inaweka kando ushindi wao wa Kombe la Dunia 2014 wakati safari ya kufuzu katika dimba la Euro 2016 ikianza dhidi ya Scotland mjini Dortmund. Kocha Loew anataka kuanza mechi hiyo ya Kundi D kwa ushindi.

https://p.dw.com/p/1D7kM
Länderspiel Deutschland gegen Argentinien
Picha: Reuters/I. Fassbender

Ujerumani iko katika kundi moja na Ireland, Poland, Georgia na Gibraltar. Miezi miwili tu baada ya kunyakua Kombe la Dunia nchini Brazil, ambalo ndilo lao la nne, Ujerumani sasa imegeuka kuwa timu inayofanywa mabadiliko. Wachezaji watatu Philipp Lahm, Per Mertesacker na Miroslav Klose wametundika daluga na saa nafasi zao lazima zijazwe, napia majeraha yamekikumba kikosi cha Loew.

Nahodha mpya Bastian Schweinsteiger, viungo Julian Draxler, Mesut Oezil na Sami Khedira, na mabeki Shkodran Mustafi, Mats Hummels Na Marcel Schmelzer wote wako nje katika mechi dhidi ya Scotland.

Loew pia anastahili kuamua kama atampa fursa nyingine mshambuliaji Mario Gomez ambaye alionekana kukosa shabaha mbele ya lango katika mechi ya kirafiki wiki hii dhidi ya Argentina ambayo walilimwa magoli manne kwa mawili. Mshambuliaji huo wa Fiorentina alizomewa na mashabiki lakini Loew alimtetea akisema atahitaji kuendelea kufanya mazoezi baada ya kukosekana uwanjani kwa miezi saba kwa ajli ya jeraha. Kocha huyo hata hivyo alisema mechi hiyo ya kirafiki iliwapa nafasi ya kujiandaa zaidi wka mechi ya kesho.

Kama Gomez hataanza mechi hiyo, basi magoli yatatoka kwa safu imara ya wachezaji wa viungo kama vile Thomas Mueller, Marco Reus, Andre Schuerrle na Lukas Podolski.

Mwandishi:Bruce Amani/AFP/DPA/reueters
Mhariri:Josephat Charo