1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yafurahia uchumi unaokua

13 Agosti 2010

Pato jumla la ndani la Ujerumani limeongezeka kwa asilimia 2.2 katika robo ya pili ya mwaka huu wa 2010 kulinganishwa na miezi mitatu ya mwanzo.

https://p.dw.com/p/OnMN
Bundeswirtschaftsminister Rainer Bruederle (FDP), vorne, spricht am Donnerstag, 01. Juli 2010, im Bundestag in Berlin vor Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) und Aussenminister und Vizekanzler Guido Westerwelle (FDP). (apn Photo/Berthold Stadler) --- German Minister for economy Rainer Bruederle (FDP), front, speaks in front of chancellor Angela Merkel (CDU) and German foreign minister Guido Westerwelle (FDP) at the German parliament Bundestag in Berlin, Germany, Thursday, July 01, 2010. (apn Photo/Berthold Stadler)
Waziri wa Uchumi wa Ujerumani,Rainer Bruederle.Picha: AP

Hiyo ni kwa mujibu wa idara ya takwimu ya Ujerumani mjini Wiesbaden. Mwanzoni,habari hizo zinavutia, kwani ukuaji wa kiuchumi kama huo, ulitokea miaka ishirini na tatu iliyopita. Tangu mwanzoni mwa juma hili, takwimu mpya zimetoa matumaini makubwa kuhusu mauzo ya nje ya Ujerumani. Kuambatana na hesabu hizo mpya, biashara ya bidhaa za Kijerumani yaani "Made in Germany" inakaribia kiwango cha kabla ya kutokea msukosuko wa kiuchumi duniani. Maendeleo hayo ni muhimu kwa soko la ajira, kwani inavyoelekea idadi ya wakosa ajira itapungua na kufikia chini ya milioni tatu katika majira ya mapukutiko.

Yote hayo huashiria kuwa uchumi wa Ujerumani sasa upo njiani kuimarika. Hata hivyo kuna sababu tatu za kuwa na tahadhari. Uchumi wa Ujerumani upo nusu njia tu ya kufikia kiwango imara cha zamani: pili, mauzo ya nje ndio yaliyochangia ukuaji huo kwa sehemu kubwa. Matumizi ya ndani yangali yakiyumba.Na kutegemea biashara ya nje ni hatari. Kwani msukosuko wo wote ule kutoka nje kama vile mzozo wa sarafu au kuongezeka kwa bei ya mafuta- ni mambo yatakayoweza kuathiri ukuaji huo kama ilivyotokea wakati wa msukosuko wa kiuchumi miaka ya hivi karibuni.

Sababu ya tatu ya kutahadhari ni hatari ya kuzama katika furaha kubwa. Kwani wanauchumi wa Kijerumani wakifurahia uchumi unaoimarika, huko Marekani Mwenyekiti wa Benki Kuu ya nchi hiyo Ben Bernanke anasababisha wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya uchumi nchini mwake. Na Japan nako,hakuna kingine kinachozungumzwa isipokuwa ukuaji dhaifu wa uchumi na mpango wa kudhibiti matumizi. Je, kuna hatari ya uchumi wa nchi hizo mbili kudorora upya. Na kutoka China, kuna ishara kuwa kasi ya ukuaji wake wa kiuchumi inapungua. Hatimae Ulaya iliyo na tatizo kubwa la madeni,ambako Ujerumani ni muuzaji mkubwa wa bidhaa zake. Je, itakuaje ikiwa hakuna atakaemudu kulipia bidhaa hizo?

Kwa hivyo, Ujerumani ina changamoto ya kufirikia upya mfumo wa uchumi wake.Badala ya kutegemea zaidi biashara ya mauzo ya nje,iimarishe biashara yake ya ndani.

Mwandishi: Böhme,Henrik/ZPR

Mhariri: Charo,Josephat