1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yahidi kuisadia Sudan

Aboubakary Jumaa Liongo30 Novemba 2010

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani, Guido Westewelle, ameahidi msaada wa fedha kwa Sudan ili nchi hiyo iendeshe kwa haki zoezi la kura ya maoni itakayoamua iwapo eneo la Sudan Kusini lijitawale au la.

https://p.dw.com/p/QM0R

Kura hiyo itafanyika tarehe 9 Januari mwakani.

Akizungumza katika mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na mataifa ya Afrika ambao umemalizika leo huko Tripoli, Libya, Westerwelle amesema matokeo kuaminika ya kura hiyo ya maoni yatakuwa na faida kwa eneo la Afrika.

Amesema iwapo Sudan Kusini itaamua kujitenga, basi nchi yake itatoa misaada mingi ya kimaendeleo kwa ajili ya taifa hilo jipya.Lakini pia amesisitiza misaada hiyo itatolewa kwa Sudan Kaskazini.

Masuala muhimu yaliyojadiliwa katika kikao hicho cha siku mbili ,ni pamoja na suala la wakimbizi wa Afrika wanaokimbilia Ulaya, malengo ya maendeleo kwa Afrika, mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na biashara.