1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaidhinisha kupunguza kaboni dayoksaidi

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXYp

Serikali ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel imeidhinisha mradi wenye thamani ya mabilioni ya Euro ili kupunguza uzalishaji wa gesi zinazochafua mazingira.Mradi huo wenye vipengele 14 unatoa mwito wa kupunguza gesi hizo kwa asilimia 36 ifikapo mwaka 2020,kulinganishwa na vile viwango vya mwaka 1990.

Miongoni mwa hatua hizo ni kupunguza uzalishaji wa gesi ya kaboni dayoksaidi kwa tani milioni 220,kutumia zaidi nishati mbadala na majengo yatapaswa kufanyiwa ukarabati ili kusaidia kupunguza matumizi ya nishati.