1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yajinoa kuchuana na Gibraltar

Admin.WagnerD11 Novemba 2014

Mechi za kufuzu katika dimba la kombe la mataifa ya Ulaya, Euro 2016 nchini Ufaransa zitachezwa tena kuanzia Ijumaa wiki hii, ambapo Ujerumani inakwaana na timu changa ya Gibraltar

https://p.dw.com/p/1Dl8m
Joachim Loew Kleine Kampfbahn
Picha: Getty Images/Alex Grimm

Kisha vjana hao wa kocha JoachimLoew watashukadimbani na mabingwa wa Ulaya Uhispania katika mchezo wa kirafiki mjini Vigo siku ya Jumanne wiki ijayo. Wakati huo huo mchezaji wa kati wa Chelsea London na timu ya taifa ya Ujerumani Die Mannschaftt Andre Schuerrle hatakuwamo katika kikosi hicho cha kocha Joachim Loew baada ya kukubaliana kwamba abakie mjini London kuangalia juu ya afya yake baada ya kuugua mwezi uliopita.

Wakati huo huo mchezaji wa kati wa Ufaransa Blaise Matuidi amelazimika kujitoa kutoka katika kikosi hicho kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Albania na Sweden baada ya kuvunjika mfupa wa mkono wake jana katika pambano dhidi ya Olympique Marseille.

Kocha wa Ugiriki Claudio Ranieri atalazimika kufanya mabadiliko mawili katika kikosi chake kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Euro 2016 dhidi ya visiwa vya Faroe baada ya wachezaji wake kuumia. Mlinzi wa Borussia Dortmund Sokratis Papastathopoulos amevunjika mfupa mdogo wa mguu wake wa kulia na ataweza kurejea uwanjani baada ya wiki mbili wakati Costas Fortounis wa Olympiakos pia ameumia.

Kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Italia Antonio Conte amemteua tena Mario Balotelli kurejea kundini kwa mchezo dhidi ya Croatia siku ya Ijumaa. Mchezo wa mwisho wa Balotelli katika kikosi hicho cha Azzurri ulikuwa katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil katikati ya mwaka huu.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afp / dpae / rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman