1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yapata ushindi mnono

13 Oktoba 2012

Ujerumani ilijitupa dimbani Ijumaa(12.10.2012)dhidi ya Ireland ambapo wachezaji walivaa kitambaa cheusi mkononi kwa heshima ya mwanasoka wa zamani wa Ujerumani Helmut Haller aliyefariki Alhamisi akiwa na umri wa miaka 78

https://p.dw.com/p/16PQP
Germany's Marco Reus (L) in action next to his team mate Miroslav Klose (C) and Ireland's Seamus Coleman (R) during the FIFA World Cup 2014 qualifying soccer match between Ireland and Germany at Aviva stadium in Dublin, Ireland, 12 October 2012. Photo: Federico Gambarini/dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Marco Reus akifunga bao la kwanza dhidi ya IrelandPicha: picture-alliance/dpa

Ilikuwa maombolezo ambayo yameleta hamasa kwa kikosi kizima cha Joachim Loew katika uwanja wa Aviva mjini Dublic. Kikosi cha timu ya Ujerumani kiliisambaratisha Ireland kwa mabao 6-1, kipigo hicho kikielezewa kuwa cha juu kabisa kocha mkongwe na maarufu barani Ulaya , Giovanni Trapatoni kukipata akiwa kocha wa timu ya taifa ya Ireland.

Germany's coach Joachim Loew (L) talks to Ireland's coach Giovanni Trapattoni prior to the FIFA World Cup 2014 qualifying soccer match between Ireland and Germany at Aviva stadium in Dublin, Ireland, 12 October 2012. Photo: Federico Gambarini/dpa
Kocha wa Ujerumani Loew akisalimiana na Giovanni Trapatoni wa IrelandPicha: picture-alliance/dpa

Akataa kung'atuka

Hata hivyo kocha huyo raia wa Italia, amesisitiza kuwa hataitupa mkono timu hiyo, na kuacha kazi yake licha ya kupata kipigo kikubwa kama hicho nyumbani. Ujerumani imefanya kazi nyepesi jana kuishinda Ireland katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil , kwa ushindi huo wa mabao 6-1 kupitia mabao yaliyowekwa wavuni na Marco Reus na mchezaji wa akiba Toni Kroos, pamoja na Miroslav Klose na Mesut Ozil.

Kocha huyo ambaye yuko katika mbinyo mkali baada ya Ireland kufanya vibaya katika michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Ulaya 2012, amekataa ushauri kuwa sasa umefika wakati wa yeye kuachia ngazi.

Nitabaki, amesema Trapatoni , kwasababu ninajihisi fahari na timu hii. Sio kwa ajili ya pesa, ni kutokana na jinsi ninavyojisikia fahari katika kazi hii, ameongeza Trapatoni.

Trapatoni amekiri kuwa Ireland ilikuwa katika hali mbaya , na amekana kuwa majaliwa yake ya kuwa katika timu hiyo yanategemea matokeo katika mchezo baina ya timu hiyo na visiwa vya Faroe siku ya jumanne.

Tulipanga kupata mabao mengi katika mchezo huu, amesema Marco Reus akizungumza na kituo cha televisheni cha ZDF. Kocha alitutayarisha vizuri. Tuliudhibiti mchezo vizuri na magoli ya kuongoza ya kipindi cha kwanza yalitupa nguvu.

Hispania bado inatisha

Hispania ilionyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali, pale walipolisalimia mara nne lango la Belarus na kuacha kilio mjini Minski, baada ya timu hiyo kupata ushindi mnono wa mabao 4-0. Mchezo huo hata hivyo haukuoneshwa nchini Hispania na televisheni kwa kuwa hakuna kituo cha televisheni kilichokuwa tayari kulipa fedha za udhamini zilizotakiwa na kampuni yenye haki za kuonyesha mchezo huo Sportfive.

Goli la dakika ya 75 lililofungwa na Zlatan Ibrahimovic lilisaidia Sweden kupata ushindi wa taabu wa mabao 2-1, dhidi ya visiwa vya Faroe, baada ya kuwa nyuma kwa bao 1-0, wakati Italia ilikuja juu katika kipindi cha pili na kuishinda Armenia kwa mabao 3-1.

Paris St Germain's Zlatan Ibrahimovic celebrates his first goal during their Champions League soccer match against Dynamo Kiev at the Parc des Princes stadium in Paris, September 18, 2012. REUTERS/Benoit Tessier (FRANCE - Tags: SPORT SOCCER)
Zlatan Ibrahimovic mshambuliaji wa SwedenPicha: Reuters

Uingereza ilifanya kazi ya ziada na kufanikiwa kushinda kwa mabao 5-0 dhidi ya San Marino uwanjani Wembley, wakati kocha wa zamani wa Uingereza Fabio Capello alifurahishwa na kikosi chake kipya cha Urusi baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Ureno.

epa03094886 England manager Fabio Capello takes his seat in the stands for the English Premier League soccer match between Liverpool and Tottenham at Anfield in Liverpool, Britain, 06 February 2012. EPA/LINDSEY PARNABY DataCo terms and conditions apply http//www.epa.eu/downloads/DataCo-TCs.pdf +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kocha mpya wa Urusi Fabio CapelloPicha: picture-alliance/dpa

Uholanzi huenda ilitarajia mengi kuliko ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Andorra, ikilinganishwa na majirano zao Ubelgiji ambao walishinda pia kwa idadi hiyo ya mabao 3-0 dhidi ya Serbia na kuongeza matumaini yao kuwa ni timu inayopigiwa upatu kufikia fainali za mwaka 2014 nchini Brazil.

Ufaransa hoi

Japan iliishangaza Ufaransa , kwa kuipa kipigo cha bao 1-0. Kocha wa japan Alberto Zaccheroni aliwasifu wachezaji wake baada ya ushindi huo katika mchezo wa kirafiki jana Ijumaa, lakini alikiri kuwa kikosi chake kilikuwa na bahati kuweza kushinda pambano hilo.

Kwingineko Ecuador iliishinda Chile kwa mabao 3-1 ikijichimbia katika nafasi ya kuweza kufuzu kucheza fainali hizo za kombe la dunia nchini Brazil.

Nae kocha wa Afrika kusini Gordon Igesund alionyesha kutojali sana kushindwa kwa kikosi chake cha Bafana bafana kwa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Poland katika mchezo wa kujipima nguvu kabla ya timu hiyo kuingia uwanjani katika kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa mataifa ya Afrika mwakani, akisema kuwa matokeo hayo sio suala muhimu hivi sasa. Amesema kuwa mchezo huo ni moja katika michezo ya kukinoa kikosi chake na hakuna na haja zaidi ya matokeo.

Mwandishi: Sekione Kitojo

Mhariri: