1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yashusha pumzi baada ya SPD kusema "Ndio"

Oumilkheir Hamidou
5 Machi 2018

Hali ni bayana mjini Berlin. Marchi 14 Angela Merkel ataapishwa kwa mara ya 4 kuwa kansela . Na baraza jipya la mawaziri pia linapata sura. Baada ya CDU, na CSU SPD wanasema majina ya mawaziri yatatangazwa wiki inayokuja

https://p.dw.com/p/2thk8
Deutschland | SPD-Basis stimmt für GroKo | Pressekonferenz im Willy-Brandt-Haus
Picha: picture-alliance/Pacific Press/S. Kuhlmey

 

Rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anatarajiwa kumpendekeza bungeni hii leo, mwenyekiti wa chama cha Christian Demoratic Union-CDU, Angela Merkel achaguliwe tena kuwa kansela. Zoezo kamili la kuchaguliwa Merkel na kuapishwa baraza jipya la mawaziri linapangwa kuzekelezwa Marchi 14 inayokuja.

Kura ya ndio ya SPD imewashusha pumzi sio tu wana SPD na wahafidhina wa CDU/CSU, bali pia rais wa shirikisho Steinmeier."Ni jambo la maana kwa nchi yetu, kwamba hali hii ya kutokuwa na uhakika wala yakini sasa imetoweka."Amesema rais wa shirikisho.

Mkuu wa kundi la wabunge wa SPD, Andrea Nahles baada ya SPD kutamka
Mkuu wa kundi la wabunge wa SPD, Andrea Nahles baada ya SPD kutamkaPicha: picture alliance/dpa/K. Nietfeld

Ujerumani yashusha pumzi baada ya SPD kusema ndio

 Katibu mkuu wa chama cha kansela Merkel, CDUAnnegret Kramp-Karrenbauer ana matumaini mema anasema:"Tutashirikiana vizuri bila ya shaka na SPD. Wamehapata uungaji mkono mpana wa mashinani. Tuna mkataba wa serikali ya muungano uliofafanuliwa vyema. Huo ndio msingi wa majukumu yetu, na unabidi ufuatwe. Zaidi ya hayo kuna uwanja mpana uliosalia na ambao kila chama kinaweza kuutumia kuendeleza mipango yake wenyewe."

Wakati huo huo viongozi wa vyama hivyo vitatu, CDU/CSU na SPD, wanakutana, kila mmoja upande wake kujadiliana kuhusu hatua za mwisho mwisho za kuunda serikali. Viongozi wa CDU wanakutana mchana huu mjini Berlin. Sambamba na hayo viongozi wa CSU wanakutana nao mjini Munich kuzungumzia nani wakabidhiwe wadhifa gani katika serikali mpya ya muungano. Duru za karibu na mkutano huo zinasema Horst Seehofer atajiuzulu Marchi 13 kama waziri mkuu wa jimbo la kusini la Bavaria . Seehofer anatarajiwa kukabidhiwa wizara ya mambo ya ndani katika serikali mpya.

Kaimu waziri wa mambo ya nchi za nje Sigmar Gabriel
Kaimu waziri wa mambo ya nchi za nje Sigmar GabrielPicha: Getty Images/AFP/C. Bilan

Hatima ya Sigmar Gabriel kama waziri wa mambo ya nchi za nje haijulikani

SPD wanapanga kutangaza majina ya watakaokabidhiwa nyadhifa za mawaziri siku zinazokuja. Jumla ya wizara sita zitaongozwa na SPD miongoni mwao ni wizara ya mambo ya nchi za nje, fedha na ajira. Kinachojulikana kwa uhakika ni kwamba mwenyekiti mteule wa SPD, Olaf Scholz ndie atakaekuwa naibu kansela na kukabidhiwa wizara ya fedha. Kama Sigmar Gabriel ataendelea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje bado haijulikani."Serikali mpya ya muungano wa vyama vikuu-GroKo inabidi iwajibike zaidi" amesema Jens Spahn wa chama cha CDU.Vyama vya CDU/CSU na SPD vimepoteza idadi kubwa ya wapiga kura, la muhimu kwa sasa ni kurejesha imani ya wapiga kura amesisitiza.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa

Mhariri:Yusuf Saumu