1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yataka mabadiliko ya kidemokrasia nchini Misri

Abdu Said Mtullya2 Februari 2011

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Westerwelle amesema lazima demokrasia iletwe haraka nchini Misri.

https://p.dw.com/p/109GZ
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle .Picha: AP

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema lazima mabadiliko ya kuelekea kwenye demokrasia yafanyike haraka nchini Misri.Waziri Westerwelle ameyasema hayo leo mjini Berlin alipokuwa anazungumzia juu ya matukio ya nchini Misri.

Kutokana na mgogoro wa kisasa unaondelea nchini Misri, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Westerwelle ametoa mwito wa kufanyika mabadiliko ya haraka ya kuelekea katika demokrasia. Waziri Westerwelle amesema siyo sawa kuuchelewesha mchakato wa kuyaleta mabadiliko. Amesema wakati wa kufanyika mazungumzo juu ya kuleta mabadiliko ya kidemokrasia ni sasa.Waziri huyo amezitaka pande zinazohusika zijiwajibike katika kudumisha amani ya ndani na ya nje.

Akizungumzia juu ya kauli ya rais Mubarak kwamba rais huyo hatogombea kipindi kingine cha urais waziri huyo wa Ujerumani amesema kuwa uamuzi wa rais huyo ni hatua inayofungua njia ya kuleta mwanzo mpya wa kisiasa nchini Misri.

Waziri Westerwelle ameyaunga mkono maandamano ya amani yanayofanywa na watu wa Misri.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani pia amezungumzia juu ya mchango unaoweza kutolewa na Umoja wa Ulaya katika Misri ya siku za usoni.Amesema kuwa Umoja huo utasaidia katika ujenzi wa mahakama, taasisi za kisiasa na pia utasaidia katika maandalio ya uchaguzi.

Waziri Westerwelle amesema serikali ya Ujerumani inawasiliana na pande zote zinazohusika ikiwa pamoja na serikali ya Misri na ,mpinzani wa rais, bwana Mohammed Elbaradei . Mwandishi/Kiesel Heiner/

Tafsiri/Mtullya abdu/

Mhariri/.Othman Miraji/