1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatoa mwito wa amani Kenya

Abdu Said Mtullya8 Machi 2013

Mshauri wa masuala ya Afrika katika serikali ya Ujerumani Nooke amesema miradi ya maendeleo baina ya nchi yake na Kenya itadumishwa hata baada ya matokeo ya uchaguzi.Amesema hayo katika mahojiano na Andrea Schmidt wa DW

https://p.dw.com/p/17tvi
Mshauri wa Kansela wa Ujerumani juu ya masuala ya Afrika Günter Nooke
Mshauri wa Kansela wa Ujerumani juu ya masuala ya Afrika Günter NookePicha: DW/P. Henriksen

Watu nchini Kenya wanayasubiri kwa hamu,kwa hofu,lakini pia kwa matarijio ,matokeo ya uchaguzi mkuu ambapo wagombea wakuu ni Uhuru Kenyatta na Raila Odinga. Mpaka sasa hali ni shwari.Lakini watu nje ya Kenya wanaitathmini vipi hali hiyo.

Günter Nooke,mshauri wa Kansela wa Ujerumani juu ya masuala ya Afrika amesema katika mahojiano hayo kwamaba japo ni vigumu kufuatilia matukio yote ya nchini Kenya kutokea Berlin amevutiwa na ukweli kwamba wananchi wote wa Kenya waliotaka kutumia haki yao ya kupiga kura walipata fursa ya kufanya hivyo

Amesema ameshangazwa lakini kwa mazuri, kwamba wote waliotaka kupiga kura walikuwa na uwezekano wa kipiga kura.Ameeleza kuwa kimsingi inapasa kusema kwamba ni jambo zuri ikiwa wananchi wanapewa fursa ya kushiriki katika kupitisha maamuzi ya kisiasa

Kenyatta pia anayo haki mahakamani:

Katika mahojiano hayo bwana Nooke pia amejibu swali juu ya mgombea wa muungano wa "Jubilee" Uhuru Kenyatta anaekabiliwa na mashtaka ya kutenda uhalifu dhidi ya ubinadamu.Jee itawezekana kushirikiana naye endapo atakuwa Rais wa Kenya? Mshauri wa Kansela wa Ujerumani juu ya masuala ya Afrika bwana Nooke amejibu kwa kusema kwamba Kenyatta bado anakabiliwa na mashtaka na siyo hukumu. Nooke ameeleza kuwa pana tofauti na Rais wa Sudan , Al Bashir. Nooke amesisitza kwamba kama ilivyo kanuni, katika mahakama zote, Kenyatta pia anayo haki mbele ya Mahakama Kuu ya mjini The Hague, ambayo inapaswa kuthibitisha iwapo ametenda uhalifu.

Hata hivyo amesema pana tatizo,kwa sababu Ujerumani inaiunga mkono Mahakama Kuu ya mjini the Hague."

Bwana Nooke ameeleza kwamba hali inaweza kuwa ya utata ikiwa Kenyatta atakuwa Rais huku anakabiliwa na mashtaka.Lakini amesema itafaa kusubiri mpaka wakati utakapofika.

Bwana Nooke pia amezungumzia juu ya mchango wa jumuiya ya kimataifa katika kuwashinikiza wagombea wakuu nchini Kenya ili wayakubali matokeo ya uchaguzi. Bwana Nooke amesema Ujerumani inawatakia Wakenya amani. Amesema wote wanapendelea kuona mazingira pasipo na umwagikaji wa damu. Amekumbusha juu ya matukio yaliyofuatia uchaguzi wa mwaka wa 2007 madhara ya matukio hayo katika maendeleo ya watu na ya uchumi wa nchi.

Tahadhari dhidi ya uzushi:

Hata hivyo bwana Nooke ametahadharisha dhidi ya kuendekeza uvumi.Ametoa mwito pia kwa waangalizi wa uchaguzi wa kuzingatia ukweli.Mshauri huyo wa masuala ya Afrika katika serikali ya Ujerumani amesema kuwa Ujerumani kwa kila hali itajaribu kuidumisha miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa watu wa Kenya.

Mwandishi:Andrea Schmidt.

Tafsiri:Mtullya Abdu.

Mhariri:Yusuf Saumu