1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaukaribisha uamuzi wa rais Obama kuhudhuria mkutano wa copenhagen

Sekione Kitojo6 Desemba 2009

Ujerumani imefurahishwa na uamuzi wa rais Obama kuhudhuria siku ya mwisho ya mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa huko Copenhagen

https://p.dw.com/p/KrAl
Rais wa Marekani Barack Obama atahudhuria kikao cha mwisho katika mkutano wa hali ya hewa mjini Copenhagen .Picha: AP

BERLIN

Ujerumani imeukaribisha uamuzi wa Rais Barack Obama kuhudhuria siku ya mwisho ya mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa huko Copenhagen. Awali Obama alipangiwa kuhudhuria kikao cha tarehe 9, lakini sasa atakuwepo tarehe 18, wakati viongozi wengi wa dunia watakuwepo huko Copenhagen.Waziri wa mazingira wa Ujerumani, Norbert Roettgen aliliambia gazeti la BILD, uamuzi wa Obama ulikuwa ishara kamili, rais huyo wa Marekani alitaka ufanisi katika kupatikana kwa mpango wa kupunguza gesi zinazochafua mazingira. Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mazingira, Achim Steiner alisema uamuzi wa Obama unaashiria kuwa maafikiano yanawezekana. Inatarajiwa mkutano wa Copenhagen utaafikia makubaliano mapya yatakayochukua mahali pa makubaliano ya Kyoto yanayomalizika muda wake 2012.