1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumuishaji wa Waislamu nchini Ujerumani

25 Juni 2009

Wajumbe wote wanataka kusonga mbele na mkutano wa Kiislamu chini ya jukwaa la serikali ya shirikisho. Mdahalo huo pamoja na Waislamu nchini Ujerumani unafanyika mjini Berlin.

https://p.dw.com/p/IayL
Teilnehmer der 1. Deutschen Islam Konferenz sitzen am Mittwoch (27.09.2006) in der Orangerie des Schlosses Charlottenburg in Berlin am Konferenztisch. Bundesinnenminister Wolfgang Schäuble eröffnete die erste Deutsche Islam Konferenz zu der Vertreter der Muslime und des Staates eingeladen wurden. Foto: Wolfgang Kumm dpa/lbn +++(c) dpa - Report
Mkutano wa kwanza wa Kiislamu nchini Ujerumani uliofunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble 27.09.2006 mjini Berlin.Picha: picture-alliance / dpa

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa hivi karibuni, kiasi ya Waislamu milioni 4.3 wanaishi nchini Ujerumani. Miongoni mwao ni wachache wanaohisi kuwa wanawakilishwa na jumuiya mbali mbali za Kiislamu nchini Ujerumani zinazotuma wajumbe wake kushiriki katika mkutano wa Kiislamu unaosimamiwa na serikali kuu ya Ujerumani mjini Berlin.

Mkutano huo ni jaribio la kwanza la kitaifa kujadili matatizo na masuala ya kuwajumuisha wakazi wa Kiislamu na kufanya marekebisho panapowezekana. Wajumbe wote wanaohudhuria mkutano unaofanyika leo hii mjini Berlin wanaunga mkono mdahalo huo.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble alipoitisha mkutano wa Kiislamu hiyo miaka mitatu iliyopita,alidhamiria kuanzisha mdahalo wa dhati pamoja na Waislamu wanaoishi Ujerumani na kuwashirikisha katika midahalo ya kisiasa kuhusu dini ya Kiislamu nchini Ujerumani.Wakati huo waziri Scäuble alisema:

"Dini ya Kiislamu ni sehemu ya jamii ya Ujerumani na Ulaya.Pia ni sehemu ya wakati wa hivi sasa na siku za usoni.Waislamu wanakaribishwa Ujerumani.Watumie vipaji vyao kuiendeleza nchi hii."

Tangu miaka mitatu,wajumbe 15 wa serikali na waakilishi 15 kutoka jamii za Kiislamu wanajadiliana katika makundi matatu.Kundi moja linashughulikia masuala ya demokrasia na maadili:kundi jingine linahusika na sekta ya uchumi na vyombo vya habari na kundi la tatu linashughulikia masuala ya dini kuambatana na katiba ya Ujerumani.

Mwanasheria Mathias Rohe alie mtaalamu wa masuala ya Kiislamu ni mjumbe katika kundi hilo la tatu.Kwa maoni yake kazi kuu ya kundi hilo ni vipi Waislamu wanaweza kujiandaa kwa njia ambayo serikali itaweza kwa pamoja kupitisha maamuzi yanayopaswa kutekelezwa.Hilo ni muhimu ili serikali za majimbo na mitaa ziwe na utaratibu mmoja zinaposhughulikia jamii zao za Kiislamu.

Mwandishi:Dorothea Jung/ZR/ P.Martin

Mhariri: M.Abdul-Rahman◄