1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukame wazidi kuathiri mamilioni Pembe ya Afrika

Martin,Prema17 Julai 2011

Afisa mwandamizi wa Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, ameonya juu ya kuzidi kuwa mbaya kwa hali ya mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa kutokana na ukame ulioenea katika Pembe ya Afrika.

https://p.dw.com/p/RaIL
Kenya: drought leaves dead and dying animals in northen KenyDead and dying animals at the Dambas, Arbajahan, Kenya, which has dried up due to successive years of very little rain. Africa's climates have always been erratic but there is evidence that global warming is increasing droughts, floods and climate uncertainty and unpredictability. Picture credit: Brendan Cox / Oxfam Picture date: 15 January 06 +++CC / Brendan Cox / Oxfam+++ am 10.1.2004 aufgenommen am 23.11.2010 ins CMS gestellt Lizenz: http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/2.0/deed.dea
Ukame katika Pembe ya Afrika umeteketeza mifugo.Picha: CC / Brendan Cox / Oxfam

Mkurugenzi Anthony Lake amesema, mvua hazitazamiwi kunyesha karibuni na msimu wa mavuno unakaribia. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, maelfu ya watu wameondoka Somalia kwa sababu ya ukame ulioathiri pia mamilioni ya watu na kuteketeza mifugo katika nchi jirani za Kenya,Ethiopia na Djibouti. Ujerumani imeahidi kutoa Euro milioni 5 kuwasaidia wahanga wa ukame katika kambi za ukimbizi.