1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi Mashariki ya kati ni mdogo kumudu ajira kwa vijana

Amina Mjahid
2 Mei 2018

Shirika la fedha la kimataifa IMF lmesema robo ya vijana wa Mashariki ya Kati hawana ajira, likionya iwapo mabadiliko hayatafanyika, mamilioni ya vijana wanaoingia katika soko la ajira kila mwaka huenda wasipate ajira.

https://p.dw.com/p/2x3TC
Kuwait Öl-Industrie
Picha: Getty Images/AFP/Y. Al-Zayyat

Shirika hilo la IMF limesema viwango vya ukuaji katika eneo hilo havitaweza kutoa nafasi za kazi zinazohitajika ili kupunguza idadi ya waliyokosa ajira, jambo lililokuwa muhimu au sababu kuu ya kufanyika maandamano makubwa ya kutaka mageuzi katika nchi za kiarabu mwaka 2011.

Kiwango cha ukuaji wa uchumi katika nchi zinazosafirisha mafuta nje ya nchi kilifikia asilimia 5 mwaka 2016 lakini kikapungua hadi asilimia 1.7 mwaka 2017.  Aidha IMF inakadiria kuongezeka kwa kiwango hicho kufikia asilimia 3 mwaka huu na asilimia 3.3 mwaka 2019.

Lakini kwa mataifa ya Mashariki ya kati yanayoingiza mafuta, ukuaji wa uchumi unatarajiwa kubakia imara kwa zaidi ya asilimia 4.

"Hili ni eneo changa, takriban asilimia 60 ya idadi ya watu ni chini ya miaka 30 na kiwango cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana kinazidi asilimia hiyo 30, hali hii inapaswa kushughulikiwa haraka," alisema Jihad Azour, mkurugenzi wa shirika la fedha la kimataifa  IMF idara ya Mashariki ya Kati na Asia ya kati.

Bildergalerie Ägypten Dritter Jahrestag des Aufstandes 25. Januar 2014
Baadhi ya waandamanaji nchini Misri wakati wa maandamano makubwa ya mageuzi yaliyokumba mataifa ya kiarabuPicha: AFP/Getty Images

Azour, aliyezungumza na shirika la habari la Associated Press wakati wa uzinduzi wa ripoti yao mpya, alisema mataifa katika eneo hilo yanapaswa kuendeleza mfumo wa mageuzi. Kwa sasa IMF inazitolea mwito serikali kuboresha ujuzi  wa watu wake na kutoa nafasi kwa sekta binafsi kufikia fedha. 

Shirika hilo la IMF pia limezihimiza waingizaji na wauzaji wa mafuta katika emeo hilo la Mashariki ya kati kupunguza matumizi makubwa ya fedha na kutafuta vyanzo vipya vya mapato kwa kuanzishaulipaji wa kodi na kutoa ruzuku.

Mwaka huu Saudi Arabia, Nchi ya falme za kiarabu, na Bahrain zinazojulikana kama nchi zisizotoza kodi ilianzisha asilimia 5 ya kodi ya ongezeko la thamani kwa bidhaa zake na huduma ili kuongeza uchumi wa nchi. Lakini licha ya juhudi hizi kando na juhudi hizi upungufu wa viwango vya fedha kwa mataifa sita yanayouza mafuta katika eneo la Guba ikiwemo ikiwemo Algeria, Iraq Iran Yemen na Libya inatazamiwa kufikia dola bilioni 294 kwa miaka mitano ijayo.

Huku hayo yakiarifiwa ripoti ya IMF inasisitiza kuwa mabadiliko katika eneo hilo yanapaswa kujumuisha ongezeko la uazi na uadilifu katika taasisi imara pamoja na utawala bora. Shirika hilo linakadiria viwango vya ukuaji kufikia asilimia 4.9 miaka mitano ijayo kwa mataifa yanayoingiza mafuta katika aeneo la Mashariki ya Kati lakini ukuaji huo unabakia mdogo kupunguza viwango vya ukosaji ajira kwa vijana.

Mwandishi Amina Abubakar/AP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman