1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Ulaya ni mustakabali wetu"

26 Machi 2007

Kwenye sherehe ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuasisiwa Umoja wa Ulaya iliyofanyika mjini Berlin jana, Bi Merkel pamoja na rais wa halmashauri kuu ya Umoja huo, José Manuel Barroso na Bw. Pöttering, rais wa bunge la Ulaya, walitia saini makubaliano ya Berlin. Azimio hilo linatarajiwa kuwa ni hatua ya kwanza katika kuunda katiba mpya ya Umoja wa Ulaya. Ufuato ni uchambuzi wa mwandishi wetu wa mambo ya Ulaya, Bernd Riegert.

https://p.dw.com/p/CHHY
Fataki kwenye sherehe ya Berlin
Fataki kwenye sherehe ya BerlinPicha: AP

Ilikuwa sherehe nzuri. Jua lilileta joto, mazulia mekundu yalikuwa marefu, wanasiasa walicheka na kutoa hotuba na watu wengi walikuja kuwashangilia. Lakini ni nini sasa kitakachobaki? Jibu ni kwamba Angela Merkel, ambaye kwa sasa anachukua kiti cha urais katika Umoja wa Ulaya, alifanikiwa kuwahamasisha tena wale viongozi wa Umoja huo waliokuwa wamechoka na mambo ya Umoja wa Ulaya. Katika makubaliano ya Berlin, ambayo yanaweza kufahamika pia kwa wale ambao hawaongei lugha ya Kirasimu, nchi washirika wa Umoja wa Ulaya zimeafikiana kuunda katiba mpya hadi ifikapo mwaka wa 2009.

Bi Merkel anautaka Umoja huu uweze kuchukua hatua tena baada ya kujihusisha na masuala ya kuyajumuisha mataifa mapya. Wale wenye wasiwasi juu ya katiba ya Ulaya aliwaambia Bi Merkel kuwa tangu mwanzoni Ulaya ilisemekana kuwa ni kama ua lilo nyauka, lakini kwa maoni yake ni ua iliyostawi vizuri sana.

Hivyo, Angela Merkel alifunga goli muhimu kwa kutoa hotuba yake vizuri. Ikiwa sasa ataweza pia kuwashawishi raia wa Ulaya ambao hawana imani katika Umoja wa Ulaya, bado haijulikani. Angalau lakini Kansela huyu alitumia maneno yanayofaa kueleza msingi wa Umoja huu hapo aliposema: Tumeungana kutokana na bahati tuliyo nayo. Ulaya ni mustakabali wetu. Kuheshimiana ni lengo letu kuu.

Ya kusifu pia ni kusisitiza ushirikiano wa karibu na Marekani na katika Shirika la Kujihami ya Magharibi, NATO. Merkel alisema lazima Ulaya isitenganishwe na Urusi ambayo Ulaya inataka kujenga ushirikiano wa pamoja nayo. Hapo, Merkel alitaja mvutano juu ya mitambo ya Marekani ya kufyetua makombora ambayo inatajariwa kujengwa nchini Poland na Tcheki, ikipingwa vikali ya Urusi.

Dai la Bi Merkel kusisitiza umoja katika sera za nishati, mazingira na mambo ya kigeni ni muhimu na tena ni ukweli wa mambo. Baada ya hotuba kuisha, sasa inabidi maslahi ya nchi zote 27 washirika wa Umoja huo yaambatanishwe. Akizikosoa Sudan, Zimbabwe na Iran, Kansela Merkel aliweka wazi kuwa, Umoja wa Ulaya unataka kubeba jukumu zaidi kwenye uwanja wa kimataifa.

Sasa itategemea ikiwa viongozi wa mataifa ya Ulaya wataendelea kwenye njia hii iliyofunguliwa mjini Berlin na kukubaliana ratiba ya kuelekea kwenye katiba katika mkutano wao ujao mjini Brussels.

Zaidi sasa ni juu ya rais mpya wa Ufaransa atakayechaguliwa mwezi wa Mei. Kuhusiana na haya, Bi Merkel hana usemi. Lakini aliweka wazi kuwa ana nia ya kupalilia bustani ya Ulaya, hata ikiwa kuna upinzani. Hadi sasa anaonekana kuwa mkulima mzuri wa bustani hiyo.