1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu waendelea kuisaidia Ufilipino

12 Novemba 2013

Umoja wa mataifa umetoa wito wa kukusanywa msaada wa dola milioni 301 kuwahui wakaazi wa visiwa vya Ufilipino vilivyoteketezwa na kimbunga Haiyan kilichoangamiza maisha ya watu wasiopungua elfu kumi

https://p.dw.com/p/1AFyG
Picha: Reuters

Kwa ushirikiano pamoja na serikali tumeanzisha mpango wa vitendo unaotuwama katika chakula, afya, kusafisha, kujenga mahema na kuondowa vifusi pamoja na kuwashughulikia wale ambao ni dhaifu zaidi. Na tunataraji wafadhili wataonyesha ukarimu," amesema mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia opereshini za kiutu bibi Valerie Amos.

Müango huo utakaoendelea hadi mwishoni mwa mwezi wa Mai mwaka 2014 utagharim u dala m ilioni 301,amesema na kuongeza fedha hizo hazijumuishi dala milioni 25 zilizoahidiwa tayari na umoja wa Mataifa.

"Kwasasa ni sahida mno kuashiria msaada wa aina gani wa dhjarura unahitajika kwasababu n i sana kuyafikia maeneo ya maafa" amesema bibi Valerie Amos aliyesifu juhudi za jumuia ya kimataifa kutaka kuwasaidia wahanga wa kimbunga hicho cha Haiyan.

Mkuu wa Masuala ya Kiutu na misaada ya dharura katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos
Mkuu wa Masuala ya Kiutu na misaada ya dharura katika Umoja wa Mataifa Valerie AmosPicha: Yasser al-zayyat/AFP/Getty Images

Kwa upande wake shirika la chakula na kilimo la Umoja wa mataifa limetoa wito wa kukusanywa dala milioni 24 kusaaidia shughuli za kilimo na uvuvi-sekta mbili zilizoteketezwa moja kwa moja na kimbunga hicho. Watu karibu milioni kumi,kwa maneno mengine,asili mia 10 ya wakaazi jumla wa visiwa vya Ufilipino wamepoteza kila walichokuwa nacho..Zaidi ya watu laki sita na sitini elfu hawana mahala pa kuishi.

Kutokana na kukawia kuwasili misaada,wengi wanaanza kuyapa kisogo maeneo ya maafa.Katika uwanja wa ndege wa Tacloban watu wanasukumana kuania nafasi katika ndege za kijeshi.

Nchi kadhaa,taasisi na mashirika yasiiyomilikiwa na serikali yameahidi kusaidia kwa hali na mali.Mbali na manuari za Marekani,serikali ya mjini London imetangaza kutuma ndege namanuari,Ujerumani pia imetuma shehena ya mwanzo ya misaada.Lakini patahitajika siku kadhaa kabla ya misaada hiyo kuwafikia waliokusudiwa.

Ndege ya shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia watoto UNICEF ikisheheni tani 60 za mahema na madawa na zana za kusafisha maji inatarajiwa kuwasili Manilla sakati wowote kutoka sasa.

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/AP/AFP

Mhariri: Josephat Charo