1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UM na vita dhidi ya umasikini

26 Septemba 2008

Shabaha ya kupunguza hadi nusu umasikini hadi 2015 ni vigumu kufikiwa.

https://p.dw.com/p/FPcp

Umoja wa Mataifa mjini New York, umeamua kukusanya kiasi cha dala Bilioni 16 kwa vita vya kupambana na njaa ulimwenguni.Lakini,kwa jicho la kuifikia ile shabaha ya Milenium ya kupunguza ufukara kwa nusu hadi ifikapo 2015 ,ni kama tone tu baharini.Isitoshe, katika mjadala wake kuhusu ushirika na maendeleo kati ya nchi za viwanda za kaskazini mwa dunia na zile zinazoinukia za kusini, imebainika kuna kasoro katika kuwa mkweli. Kwani,yule atakae kupiga vita umasikini kuwa ni hatari kwa usalama na kutumia misaada ya maendeleo kama ifanyavyo Ujerumani kama sera ya kuhifadhi usalama,anabidi kuongeza fedha.

Mwishoni,mkutano huo wa Um ulikusanya kitita hicho cha dala bilioni 16 na viongozi wa kisiasa wa burdani na wa mabaneki wakajitolea ingawa kwa mdomo tu kuchangia bilioni 3 zaidi kupiga vita malaria na kiasi cha bilioni 5 nyengine kwa miradi ya elimu.

Hatahivyo, asitokee mtu kufikiria kwamba shabaha ya kupunguza umasikini duniani kwa nusu hadi ifikapo 2015 itafikiwa.Hatahivyo, hatua ya kwanza kuelekea huko imechukuliwa New York.Upumbavu ni mwito aliotoa Jeffery Sachs kuwa nchi tajiri zitimize ahadi zao za kuchangia 0.7% ya pato lao la kitaifa kusaidia maendeleo ya nchi changa tena katika kipindi hiki cha kuzorota uchumi na msukosuko wa mabaneki......

Tatizo ni jengine kabisa na linafahamika tangu miaka mingi:vita vya kupambana na umasikini vinahitaji kubadili mfumo wa misaada na sio ruzuku. Kwa kadiri Umoja wa Ulaya unalipa fidia kwa wakulima kwa nyama ya ngombe wanaosafirisha katika masoko ya nchi changa za kusini,wakulima wa mifugo ya ngombe nchini namibia hawatanyanyuka.Kwa kadiri Marekani inatoza ushuru kwa njugu nyasa na pamba kutoka afrika lakini wakati huo huo inawataka washirika wao wa biashara barani afrika kufungua milango wazi ya masoko yao kwa bidhaa zao ,maonevu yatasalia na kamwe ni vigumu kurekebishwa na bora zaidi na Shirika la Biashara Ulimwenguni.

Kwa namna hii nchi za kiviwanda za magharibi, zinapoteza dhamana zao na nchi za kusini zinabidi kujitwika binafsi dhamana hizo.Kitu gani kinachozuwia serikali za kiafrika kuagiza binafsi dawa na zana kwa bei nafuu kupiga vita maradhi ya malaria ?

Kwa jumla, mjadala kuhusu ushirikiano katika misaada ya maendeleo kati ya nchi za viwanda za kaskazini na changa za kusini, unabidi kuendeshwa kwa uaminifu zaidi.Yule anaepiga vita umasikini kwa kuwa anauona ni hatari ya kuweza kusababisha machafuko na yule anaeangalia misaada ya maendeleo mfano Ujerumani, kuwa chombo cha kulinda usalama , anapaswa kutoa fedha za kutosha kuupunguzia umma madhila .Mjadala wa aina hii, usianzie tu sera za kilimo na kumalizikia sera za uhamiaji na wimbi la wakimbizi na kuporomoka kwa dola hadi siasa kali.

Wakati huu misaada ya maendeleo mara nyingi hutumiwa kama malipo ya fidia kwa dhulma ya enzi ya ukoloni iliopita au kusaidia kukuza biashara ya nje.

Wakati wa mkutano huo wa kukusanya fedha wiki hii,taarifa ilichomoza inayobainisha njia ya aina nyengine ya misaada ya maendeleo: Shirika la Mpango wa chakula la UM (WEP ) lina azma kutoka sasa kutumia sehemu ya fedha zake za kununulia chakula cha misaada kununua moja kwa moja nafaka kwa wakulima wa Afrika na Amerika Kusini.Hivyo ni kununua kwa mkulima ambae anaishi kwa mavuno yake na kuuza ziyada lakini hana uwezo wa kuuza katika masoko ya nje.

Mabadiliko haya ya fikra na sera , yametanabahisha kuwa kutoa ruzuku na takrima ,hakusaidii kupiga vita umasikini.Ni kuendeleza tu ombna-omba.Bill na Melinda Gates pamoja na serikali ya Ubelgiji wamevutiwa mno kugharimia mradi kama huu.