1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika waanza upatanishi nchini Kenya

9 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cn7K

NAIROBI:

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na mpatanishi rais John Kufour wa Ghana amekutana, kwa mda tofauti, na rais wa Kenya Mwai Kibaki pamoja na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Hatua hii ni kujaribu kumaliza mgogoro kuhusu matokeo ya uchaguzi ambayo yameleta utata.

Odinga amemshutumu Kibaki,kushinda kwa hila ,uchaguzi wa mwezi disemba, na amekataa kukutana nae ,uso kwa uso, bila ya mpatanishi wa kimataifa. Ghasia zingine zilitokea jana katika mji wa Kisumu ambao ndio ngome ya upande wa upinzani.Ghasia hizo zilisababishwa na hatua ya Bw Kibaki kutangaza nusu ya baraza lake jipya la mawaziri kabla ya kuwasili kwa Bw John Kufour.

Watu wanaoifika 500 wamepoteza maisha yao katika ghasia za uchaguzi ingawa upande wa upinzani unasema idadi inakaribia 1,000.Karibu nusu millioni ya watu wanafikiriwa kuhama makazi yao katika hatua ya kuepuka ghasia za kikabila.