1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika yaisimamisha uanachama Cote d'Ivoire.

Halima Nyanza(ZPR)10 Desemba 2010

Umoja wa Afrika umeisimamisha uanachama Cote d'Ivoire, kufuatia mabishano yaliyozuka katika uchaguzi wa Rais kwenye nchi hiyo ya Afrika magharibi.

https://p.dw.com/p/QUo5
Rais anayemaliza muda wake Laurent Gbagbo ambaye bado anang'ang'ania madaraka.Picha: AP

Afisa mmoja wa Umoja huo, amesema Cote d'Ivoire itasimamishwa uanachama mpaka pale kiongozi wa upinzani, Alassane Ouattara atakaposhika madaraka kutoka kwa mpinzani wake rais anayemaliza muda wake Laurent Gbagbo.

Elfenbeinküste Unruhen Dezember 2010
Kikosi cha Umoja wa Mataifa kikiimarisha ulinzi nchini humo.Picha: AP

Mpaka sasa bwana Gbagbo bado anakataa kuachia madaraka, licha ya matokeo rasmi ya uchaguzi na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kusema kwamba  mpinzani wake ameshinda uchaguzi.

Viongozi wote hao, Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara, kila mmoja anadai kushinda uchaguzi huo, hali ambayo jumuia ya kimataifa imebidi kuingilia kati.