1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wamtambua Ouattara.

Halima Nyanza9 Desemba 2010

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeonya kwamba liko tayari kuweka vikwazo dhidi ya mtu yoyote ambaye atajaribu kuvuruga mchakato wa amani nchini Cote d'Ivoire.

https://p.dw.com/p/QTrU
Kiongozi wa upinzani nchini Cote d'Ivoire Alassane Ouattara.Picha: AP

Aidha baraza hilo pia limetoa wito wa pande zote kuheshimu ushindi alioupata kiongozi wa upinzani nchini humo Alassane Ouattara, kufuatia uchaguzi wa rais uliofanyika nchini humo mwezi uliopita.

Katika taarifa iliyosomwa na balozi Brooke Anderrson, ambaye nchi yake kwa sasa ndiyo inashikilia nafasi ya Urais, baraza hilo limesema linalaani juhudi zozote zitakazovuruga matakwa ya watu ama kuhujumu uaminifu wa zoezi hilo la uchaguzi.

Rais aliyemaliza muda wake Laurent Gbagbo amekuwa akikataa mpaka sasa kukabidhi madaraka kwa mpinzani wake Alassane Ouattara, ambaye ameshinda katika uchaguzi huo wa Rais.

Elfenbeinküste Wahl Laurent Gbagbo
Rais anayemaliza muda wake Laurent Gbagbo.Picha: AP

Urusi imekuwa ikikawiza jaribio la baraza hilo la usalama kumlazimisha Bwana Gbagbo kuondoka madarakani.