1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa wapanga kueneza shughuli zake nchini Iraq

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNI

New-York:

Umoja wa mataifa umeitisha mkutano wa ngazi ya juu kwa lengo la kuimarisha uchumi na usalama nchini Iraq.Mkutano huo wa mjini New York,uliosimamiwa kwa pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon na waziri mkuu wa Iraq Nouri al Maliki,umehudhuriwa na wawakilishi wa Iraq,majirani zake na mataifa fadhili.Baada ya saa mbili za majadiliano,katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amewaambia maripota “wakati umewadia wa kuchukuliwa hatua za pamoja.”Waziri mkuu wa Iraq,Nouri al Maliki amesema serikali yake “inaweza kudhamini usalama Umoja wa Mataifa utakaporefusha shughuli zake”.Umoja wa mataifa unapanga kufungua ofisi nyengine mjini Baghdad na Basra kusimamia shughuli za misaada.Umoja wa mataifa ulipunguza harakati zake nchini humo baada ya shambulio dhidi ya ofisi yake mjini Baghdad ,lililogharimu maisha ya watu 22 akiwemo pia muakilishi wake maalum Sergio Vieira de Mello.