1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa watoa wito wa misaada zaidi.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ2Y

Dhaka. Umoja wa mataifa umetoa wito wa kutolewa misaada zaidi kwa watu nchini Bagladesh ambao wameathirika na kimbunga Sidr. Mpango wa chakula duniani umeieleza hali nchini humo, siku tano baada ya kimbunga kuwa mbaya.Akizungumzia hali hiyo balozi wa Bagladesh katika umoja wa mataifa Muhammad Ali Sorcar amesema.

Watu wanaokadiriwa kufikia milioni tatu wameondolewa kutoka maeneo yao ama wamepoteza nyumba zao. Wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada wanasema kuwa ukosefu wa misaada ya chakula , maji safi ya kunywa na madawa kunaweza hivi karibuni kusababisha kuzuka kwa magonjwa. Pia kuna wasi wasi kuwa baadhi ya maeneo ya ndani bado hayajafikiwa. Jeshi la nchi hiyo limesema kuwa bado halijaweza kutoa msaada kwa asilimia 30 ya eneo la vijiji vya pwani. Kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu wapatao 3,100, na idadi ya vifo inatarajiwa kupanda.