1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA ULAYA MIAKA 50

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCG0

UMOJA WA MATAIFA:

Leo ni siku ya kupiga vita maradhi ya kifua kikuu-TB.Katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon amezitaka serikali ulimweenguni kujiunga na mpango wa gunia wa kupiga vita maradhi hayo .Alitoa mwito huo katika risala yake iliolenga kusisitiza umuhimu wa Mpango wa dunia dhidi ya kifua kikuu unaoanzia 2006 hadi 2015.

Mwito wa katibu mkuu huyu umekuja baada ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kuripoti kuwa maradhi ya kifua-kikuu yanayobishana na madawa yanazidi.

UM unakisia kifua kikuu kinaua watu 4.400 kwa siku .Maeneo yalioathiriwa sana ni Afrika,Kusini-mashariki mwa Asia,eneo la mashariki la bahari ya Miditerranean.