1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya na Karadzic

22 Julai 2008

Umoja wa Ulaya umekaribisha kutiwa nguvuni kwa karadzic na umeiwekea Zimbabwe vikwazo zaidi.

https://p.dw.com/p/EhlG

Hatua ya Serbia ya kumtia nguvuni kiongozi wa vita vya vya wa kiserbia huko Bosnia Radovan karadzic ,ni kitendo muhimu sana kinacho ifungulia njia Serbia kujiunga na umoja wa Ulaya.Hatahivyo, Belgrade imetakiwa kufanya mengi zaidi.

Pia mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya katika kikao chao hicho leo mjini Brussels,Ubelgiji wameidhinisha vikwazo vipya kwa utawala wa Rais Mugabe .

►◄,

Katika kikao chao cha leo mjini Brussels, mawaziri hao wa nje wa Umoja wa Ulaya walijishughulisha na kukamatwa kwa Radovan Karadzic na swala la zkmbabwe.

Licha ya waakilishi wa ZANUpf na upinzani MDC kukubaliana kuanza mazungumzo juu ya mustakbala wa Zimbabwe,mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya wasmeupitishia utawala wa Mugabe vikwazo vipya.Wameongeza idadi ya viongozi wanaozuwiwa kutia mguu wao Ulaya.Pia fedha na mali zao zilioko Ulaya zitazuwiwa.

Waziri wa nje wa Ufaransa Bernard Kouchner,ambae nchi yake ya Ufaransa ndio mwenyekiti wa sasa wa UU alidai kuwa vikwazo vya hapo awali vilitoa mchango mkubwa .

Bw.Kouchner, alisema pale taarifa za kukamatwa kwa Radovan karadzich zilipowasili kwenye kikao cha mawaziri wa nje wa UU hapo jana usiku kuandaa mkutano wa leo, "kila mmoja aliruka kwa furaha." "Tukiisubiri taarifa hii kwa miaka 13"-alisema kouchner,ambae nchi yake Ufaransa, ni mwenyekiti wa sasa wa UU.

Msemaji wa sera za nje wa Umoja wa ulaya Javier solana alisema kukamatwa kwa mtu aliesakwa kwa madhambi ya uhalifu wa vita usiowahi kuonekana Ulaya tangu vita vya pili vya dunia Radovan karadzic kumebainisha kwamba Serbia iko tayari kushirikiana kikamilifu na Mahakamu ya kupambana na Uhalifu ya Umoja wa Mataifa mjini The Hague.

Katibu mkuu wa shirika la ulinzi la Magharibi-NATO Jaap de Hoop Schaeffer,alipongeza kutiwa mbaroni kwa Karadzic na akaitaka Serbia kuhakikisha kupekwa kwake haraka mjini The Hague kukabili mashtaka na kuharakisha msako wa mshirika wake wa chanda na pete Mladic.

Karadzic na Mladic wameshtakiwa kwa mauaji ya umma wa hadi waislamu 8.000 wa bosnia na kuzikwa katika makaburi ya umati wa watu.

Umoja wa Ulaya ulifunga mapatano ya kuwa na uhusiano maalumu na Serbia hapo April lakini uliapa kutoyaidhinisha au kutoa nafuu zake za kibiashara hadi kwanza Serbia imeshirikiana na Mahkama hiyo ya uhalifu ya UM .

Mahusiano kati ya UU na Belgrade yametatanishwa pia na mvutano wa Kosovo, ambako kujitangazia kwake uhuru hapo februari, kulipingwa na kulaaniwa na serbia.

Katika taarifa yao waliotoa kufuatia mazungumzo yao leo mjini Brussels, mawaziri wa UU walithibitisha tena taarifa yao kuwa Serbia yaweza kuharakisha uanachama wake katika UU lakini haukutoa wakati wa kupewa hadhi za kuwa mgombea nafasi ya uanachama.

Hii ni shabaha ambayo Belgrade ikipanga kuifikia hadi mwisho wa mwaka huu.Waziri wa nje wa Finland Alexander Stubb alisema

Umoja wa Ulaya ungetaka ushahidi zaidi wa ushirikiano wa Serbia .hata waziri wa nje wa Slovenia Dimitrij Rupel,anaeiungamkono kamili Serbia kuwa mwanachama, amesema Serbia iko nusu-njia kufikia ushirikiano kamili na UU unaotakiwa.

Hilo ni sharti lililotolewa na Umoja wa ulaya hapo April mwaka huu ili kutekeleza mapatano ya kuwa na uhusiano mkubwa baina ya UU na Serbia na kuitia njiani kuelekea uanachama kamili .