1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya na wakimbizi

24 Septemba 2008

Mawaziri wa ndani wa Umoja wa Ulaya wakutana kesho kuamua hatima ya wakimbizi hasa wa kiiraqi.

https://p.dw.com/p/FOHu

Tume ya Ulaya ya maswali ya sheria inakutana kesho mjini Brussels na usoni kabisa mwa ajenda yake ni :je, na kwa aina gani Umoja wa Ulaya uwapokee wakimbizi wa kiiraqi ?

Uamuzi juu ya hatima ya wakimbizi hao uliahirishwa kupitishwa kutokana na pendekezo la waziri wa ndani , serikali ya Ujerumani iliridhia kuwapokea wakimbizi wa kiiraqi na hasa wale wa kikiristu.

Shirika linalotetea haki za binadamu -Amnesty International na lile linalowatetea wakimbizi PRO ASYL, yalidai jana mjini Berlin kuwa wakimbizi wa kiiraqi wanaohitaji ulinzi maalumu wapewe hifadhi ya kudumu humu nchini.

Kwa jicho la hali ilio bado mbaya nchini Iraq watetezi wa haki za binadamu wanadai serikali ya ujerumani na zile nyengine za umoja wa Ulaya kuharakisha kuwapokea wakimbizi wa kiiraqi na kuacha kuahirisha zaidi swali hilo.Julia Duchrow,mjumbe wa shirika la Amnesty International -tawi la Ujerumani,anaehusika na wakimbizi amesema kuwa Amnesty na pro-Asyl wamemuandikia barua yao Kanzela Angela Merkel ili kuitaka serikali ya ujerumani kubadili msimamo wake na iseme :wakimbizi wa kiiraki wapokelwe bila kuchelewa katika nchi za Umoja wa Ulaya na hasa nchini Ujerumani.

Alisema:"Sababu ya kutoa dai letu hilo ni kuwa kwa sisi hali za wakimbizi katika nchi jirani na Irak inaendelea kuwa mabaya na kurejea makwao kwa wakimbizi kama alivyoarifiwa Kanzela Angela Merkel na waziri mkuu wa Irak Al Maliki ni jambo lisilowezekana kabisa.Nchini Jordan na Syria, wanaishi kiasi cha wakimbizi milioni 2.5 na wanaishi katika hali dhaifu kabisa.Nchi hizi mbili zimezidiwa na mzigo huo mkubwa wa idadi ya wakimbizi."

Isitoshe, anaongeza bibi Duchrow kwa hali ya sasa kuendelea kuahirisha uamuzi wa kuwapokea haraka wakimbizi wa kiiraqi kutawavunja moyo sana.

Kwani anasema bibi Duchrow kwamba kuna wakimbizi wengi wanaojua wamechaguliwa tayari na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ili kuhamishiwa nchi nyengine .Kwahivyo hapo kesho isiruhusiwe kuliahirisha zaidi swali hili ili kupitisha tu wakati.Kesho septemba 25 uamuzi wa mawaziri wa ndani wa Umoja wa Ulaya unabidi kukatwa-alisisitiza .

Ikiwa uamuzi hautapitishwa,serikali ya Ujerumani ijitoe katika uamuzi wa pamoja wa Umoja wa Ulaya na iwapokee wakimbizi kwa niaba yake.Kuna ishara tayari zilizoonesha kuwa baadhi ya mawaziri wa ndani wako tayari kuwapokea wakimbizi wa kiiraqi.

Kwa jicho la shirika la haki za binadamu la Pro Asyl Ujerumani ina mudu kuwapokea wakimbizi hadi 30.000 wa kiiraki.Bingwa anaehusika na wakimbizi Bibi Duchrow alitoa pendekezo kutoka shirika la Amnesty linalokidhi masilahi ya Umoja wa Ulaya na wanachama wake.

"Kuwapokea wakimbizi wa kiiraqi kuwe hatua ya mwanzo kuelekea mpango wa viwanga maalumu vya kuja baadae kuwapokea wakimbizi kila mwaka .Lakini sio kwa wingi mkubwa kama kundi hili la kwanza la wairaki."

Kabla kikao cha kesho cha mawaziri wa ndani wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels,

vilio vinaongezeka nchini Ujerumani kudai kuwapokea haraka wakimbizi wa kiiraki .

Waakilishi tangu wa makanisa na hata wanasiasa wanaitaka serikali ya Ujerumani kutoahirisha zaidi uamuzi wake.