1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waidhinisha kikosi cha kulinda usalama wa watu wa Darfur

28 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cyq3

BRUSSELS:

Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kwa mazungumzo yanayotarajiwa kujikita katika masuala ya Serbia, Kosovo na kikosi cha Umoja wa Ulaya cha kulinda amani nchini Chad. Habari za hivi karibuni zinasema kuwa Umoja huo umeinidhinisha kikosi cha kulinda amani Darfur.Kikosi hicho, cha wanajeshi 3000, kitatumwa Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati kwa lengo la kuwalinda watu wa Darfur. Kabla ya mkutano huo,kamishna anaehusika na upanuaji wa umoja huo,Olli Rehn aliwaambia maripota kuwa Umoja wa Ulaya hivi karibuni unaweza ukatia sahini mkataba wa ushirikiano na Serbia.

Wachunguzi wanasema kuwa Umoja wa Ulaya unataka kutuma ujumbe unaovutia kwa Serbia kabla ya kufanyika awamu ya pili ya uchaguzi mkuu wa urais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa juma.Kwa wakati huohuo nchi za Umoja wa Ulaya,zinasema kuwa zitalitambua jimbo la Kosovo endapo litajitangazia uhuru wake.Uongozi wa waAlbania wanaoishi katika mkoa wa Serbia wa Kosovo wanatarajiwa kutangaza uhuru wa jimbo hilo katika mda wa wiki chache zijazo.