1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya walamikia mateso dhidi ya mashahidi wa ghasia za uchaguzi Kenya

7 Desemba 2010

Umoja wa Ulaya waitaka Kenya kuwalinda mashahidi wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na kuhakikisha wanaharakati wa haki za binadamu hawahangaishwi

https://p.dw.com/p/QRbI
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya ICC, Luis Moreno OcampoPicha: dpa - Fotoreport

Umoja wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake kufuatia visa vilivyoripotiwa kuongezeka vya kuhangaishwa mashahidi wa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi uliopita wa mwaka 2007. Hali hiyo imejitokeza wakati ambapo mahakama ya uhalifu wa kivita, ICC, iliyoko The Hague, Uholanzi inajiandaa kuyatangaza majina ya watuhumiwa wa kuipanga njama hiyo iliyosababisha maafa. Kwa mujibu wa mwakilishi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Kenya, Eric van der Linden, jumuiya hiyo inatiwa wasiwasi na ongezeko la visa vya kuwahangaisha mashahidi na wanaharakati ambao wanajitahidi kuwasaidia. Akizungumza na waandishi wa habari, mwanadiplomasia huyo ameitolea wito serikali ya Kenya kujitolea zaidi kuhakikisha kuwa mashahidi hao wanalindwa na pia watetezi wa haki hawangaishwi.

Wiki mbili zilizopita, watu wawili wanaodai kuwa mashahidi walizibadili kauli zao na kudai kuwa walilipwa ili kumchafulia jina waziri mmoja wa zamani.