1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya watoa mpango kuiokoa Ugiriki

26 Machi 2010

Waziri mkuu wa Ugiriki aridhika

https://p.dw.com/p/Mcu5
Angela Merkel atamba juu ya swali la Ugiriki.Picha: picture-alliance/dpa

Umoja wa Ulaya, umeamua kuiungamkono Ugiriki, katika msukosuko wake wa madeni:Katika siku ya kwanza ya mkutano wao wa kilele wa siku mbili mjini Brussels, wanachama 16 wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro,waliafikiana mpango wa dharura wa kuiokoa Ugiriki , uliotungwa na Ujerumani na Ufaransa kwa nchi zinazotumia sarafu ya Euro ambazo zinakumbwa na matatizo ya fedha.Kwa njia hii, inalengwa kukomesha uvumi wa kufilisika Ugiriki. Mada hasa ya mkutano huu wa kilele wa UU, iliwekwa nyuma .

Maafikiano yalikuja haraka zaidi kuliko ilivyotazamiwa ; na kanzela Angela Merkel, anaweza kuridhika na matokeo.Kwani, shauri lililopendekezwa baina ya Ujerumani na Ufaransa,ambalo liliungwamkono na wanachama wote, linaingiza kuchangia Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) mkopo wa mabilioni kwa Ugiriki, yenye madeni kupita kiasi.Isitoshe, nchi moja moja za Umoja wa Ulaya nazo zinaweza pia kuikopesha Ugiriki.

Hadi muda mfupi uliopita, Ujerumani, ilin'gangania kudai Shirika la Fedha Ulimwenguni, lichangie na kwa msimamo huo, ilijikuta pekee imetengwa na wenzake.Hata Ugiriki yenyewe, sasa inavuta pumzi na kuridhika kama waziri mkuu wake George Papandreou anavyosema,

"Umoja wa Ulaya umepiga hatua kubwa .Leo hatukuamua tu kwa ajili ya Ugiriki."

Hata rais mpya wa Umoja wa Ulaya, Herman Van Rompuy, ambae kwa mara ya kwanza anaongoza sasa mkutano wa kilele wa UU ,ameonesha kuridhika na suluhisho lililopatikana.Mpango ulioafikiwa kinyume na kuwapo kwa mchango wa UU kuiokoa Ugiriki, haukiuki sheria za Umoja wa Ulaya.Van Rompuy akasema,

"Tunatumai kwamba, hata wale wenye kuidai serikali ya Ugiriki, wametulizana sasa kuona Eneo la sarafu ya Euro (Eurozone) halijaiacha mkono Ugiriki."

Si kwa Ugiriki wala nchi nyengine mwanachama wa UU , atakaejikuta hoi na anaugua, atakaependelea kubidi kuokolewa na mpango

kama huu .Kwani, masharti ambayo yameambatanishwa na mikopo ni magumu.Kwanza, nchi zote za Ulaya, znabidi kuamua kwa pamoja kwamba nchi mojawapo yanachama, haiwezi kupewa mkopo katika masoko ya fedha.fedha zikitolewa na Shirika la fedha ulimwenguni na nchi nyengine za ulaya kuikopesha nchi kama hiyo, riba haitafidiwa.Kwahivyo, mkopo utakua wa bei ya juu sana.

Kuhusu Ugiriki, mkopo unaohitajika kuiokoa ni wa kima cha Euro bilioni 30.Katika kima hicho , Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) haliko tayari kuchangia hata nusu yake.Sasa mpango wa dharura uliopitishwa jana hakuna anaedhania utaweza kufanya kazi miongoni mwa wale waliopo mjini Brussels.

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Uhariri.Abdul-Rahman