1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMP wawaacha guzo wapinzani wao nchini Ufaransa

Oummilkheir11 Juni 2007

Chama cha rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa UMP kimejipatia wingi mkubwa wa kura baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge kumalizika jana,wadadisi wakiashiria huenda wakalidhibiti kikamilifu bunge .Wapiga kura wachache tuu lakini wameteremka vituoni.

https://p.dw.com/p/CHCu
Waziri mkuu Francois Fillon
Waziri mkuu Francois FillonPicha: AP

Chama cha UMP kimejikingia asili mia 39.54 ya kura na huenda kikakalia viti kati ya 383 na 501 kutoka jumla ya viti 577 vya bunge duru ya pili ya uchaguzi itakapomalizika June 17 ijayo.

Hayo ni kwa mujibu wa taasisi tatu za utafiti wa maoni ya umma.

Chama cha kisochialist PS-huenda kikajingia asili mia 24.73,na pamoja na washirika wake wa mrengo wa shoto wakakalia viti kati ya 60 na 170.Katika bunge lililopita UMP walikua na viti 359 na wasoshiliasti 149.

Wabunge 110 wamechaguliwa moja kwa moja katika duru ya kwanza,na mmoja tuu kati ya hao ni wa kutoka mrengo wa shoto.

Ikiwa makadiro hayo yatathibitika duru ya pili ya uchaguzi itakapoitishwa,basi Nicolas Sarkozy atakua na uhuru wa kupitisha sheria za mageuzi bungeni kama alivyowaahidi raia wa nchi hiyo.

Bunge jipya litakalosalia madarakani sawa na rais kwa kipindi cha miaka mitano, litakutana kwa kikao cha dharura June 26 kutathmini miswaada kadhaa ya sheria ikiwa ni pamoja na kodi ya mapato na usalama.

Mrengo wa kulia unashangaria ushindi huo na kuuangalia kama thibitisho la uungaji mkono wa wafaransa kwa siasa iliyoanzishwa na Nicolas Sarkozy.Waziri mkuu Francois Fillon anasema: “Baada ya uchu wa mageuzi uchaguzi wa rais ulipoitishwa,duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge imedhihirisha azma ya wafaransa kufuata mkondo mpya.Wanataka uzembe wa kale ukome na kujikomboa toka hali ya kukata tama-wanataka wapatiwe matumaini mema na kuiona nchi yao inaanza upya kusonga mbele.”

Wasoshialisti wanawataka wananchi wazindukane na kuteremka kwa wingi vituoni duru ya pili itakapoitishwa June 17 ijayo, ili kuepukana na kishindo cha madaraka yote kudhibitiwa na upande mmoja.

Mtetezi aliyeshindwa wa kiti cha urais bibi Segolene Royale anasema: "Watu kidogo tuu ndio walioteremka vituoni kutoa sauti zao.Kwa hivyo inadhihirisha kuna kitu ambacho si sawa.Sikulaumuni.Lakini ni vyema mkielewa kuna watu ambao wamekua mpaka leo wakiisubiri fursa kama hii ya kupiga kura-na wakati mwengine kufika hadi ya kuyatia hatarini maisha yao, kwa hivyo nendeni mkapige kura, kwa masilahi yenu.”

Waziri mkuu wa zamani,Jean Pierre Raffarin anaetazamiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha UMP,amesema hii leo chama hicho kinabidi kifanyiwe marekebisho ,kiwache wazi milango yake na kuwakilisha tabaka zote za wananchi kufuatia ushindi mkubwa wa uchaguzi wa bunge.