1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umwagaji damu wafikia kilele kipya Syria

Martin,Prema16 Novemba 2011

Hadi watu 90 wameuawa nchini Syria katika kipindi cha siku moja huku upinzani dhidi ya rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad ukishuhudia kilele kipya cha umwagaji damu.

https://p.dw.com/p/Rwjn
epa02881866 A grab from a handout video made available by Shaam News Network on its youtube channel on 26 August 2011, shows protesters allegedly in Homs, Syria. According to media report, Five people were killed during protests across Syria on 26 August when security personnel used force and live ammunition in a bid to disperse the rallies, activists said. Protesters have intensified their demonstrations against the government since Ramadan started on 01 August. EPA/SHAAM NEWS NETWORK/HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE. EPA IS USING AN IMAGE FROM AN ALTERNATIVE SOURCE, THEREFORE EPA COULD NOT CONFIRM THE EXACT DATE AND SOURCE OF THE IMAGE. HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Upinzani washuhudia umwagaji damu mkubwa SyriaPicha: picture alliance/dpa

Hayo ni kwa mujibu wa makundi ya haki za binadamu na wanaharakati walio uhamishoni. Wengi wa wahanga wa umwagaji damu uliotokea siku ya Jumatatu, walikuwa wanajeshi, ikidaiwa kuwa walishambuliwa na wanajeshi walioasi. Mapigano ya mara kwa mara, kati ya wanajeshi na wale walioasi yanaripotiwa kutoka mikoa ya Deraa na Idlib.

Kwa mujibu wa matamshi ya Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, nchi yake imepoteza imani katika serikali ya Syria. Akizungumza mjini Ankara, Erdogan amesema, vitendo vya ukatili vya Assad vinamhatarisha kuingia katika orodha ya viongozi wa kisiasa wanaotawala kwa mabavu. Uturuki inashinikiza kuiwekea Syria vikwazo ambavyo havitouathiri umma wa nchi hiyo. Wakati huo huo, wajumbe wa upinzani wa baraza la taifa la Syria waliokuwa ziarani Moscow, hawakufanikiwa kuishawishi serikali ya Urusi kuchukua hatua kali dhidi ya Assad.