1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN kujadilia ongezeko la bei za vyakula

Mwadzaya, Thelma28 Aprili 2008

Mkutano wa kujadilia mbinu mwafaka za kukabiliana na ongezeko la bei za vyakula na mafuta ulimwenguni umefunguliwa mjini Bern nchini Uswisi.Kikao hicho cha siku mbili kimefunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban

https://p.dw.com/p/DqDg
Mji wa Bern, UswisiPicha: picture-alliance/ dpa


Masuala muhimu yatakayojadiliwa yanajumuisha ongezeko la matumizi ya nishati mbadala itokanayo na nafaka Kikao hicho kinanuia kuvumbua mpango wa dharura wa kupambana na tatizo la ongezeko la bei za vyakula vilevile hatua za muda mrefu za utatuzi.


Wajumbe watajadilia masuala ya kulinda masoko ya vyakula na kwa upande mwingine wanaopinga hatua ya kufungua soko la kimataifa kwa biashara hiyo.Hata hivyo ongezeko la matumizi ya nishati mbadala itokanayo na nafaka limezua mitazamo tofauti wakati ulimwengu unakabiliwa na tatizo hilo.


Ongezeko la idadi ya watu ulimwenguni linalosababisha matumizi ya chakula kuongezeka hususan katika mataifa yanayoendelea ....ongezeko la kilimo cha nafaka za kutengezea nishati mbadala vilevile athari za mabadiliko ya hali ya anga vyote vimechangia katika tatizo hilo.Hayo aliysema katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon


Katibu Mkuu Ban Ki Moon alikutana na maafisa wa Shirika la Posta Ulimwenguni kisha kuanza mkutano na mashirika 27 ya Umoja wa mataifa yanahusika na miradi ya maendeleo.Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Chakula Duniani WFP Josette Sheera alihudhuria kikao hicho na kupendekeza mambo kadhaa ''Tunachosema ni kuwa katika maeneo ambayo hakuna viwango vya juu vya umasikini wakazi wabadili mifumo yao ya chakula ikiwemo kula mlo mmoja kwa wingi.Kuna haja ya kuwa na mikakati maalum itakayoshirikisha serikali na jamii ili kuwasaidia kukidhi mahitaji yao ya chakula.''



Kiongozi wa Benki ya Dunia Robert Zoellick vilevile Jacques Diouf mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Ulimwenguni FAO pamoja na Lennart Bage Mkuu wa Mfuko wa Kimataifa wa Kilimo IFAD wote walihudhuria mkutano huo.Shirika la Chakula Ulimwenguni WFP limetoa wito wa msaada wa dharura wa euro milioni laki 485 ili kununua chakula kinacholenga kukimu mahitaji ya mataifa masikini.Bwana Ban Ki Moon anatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne wakati wa asubuhi.