1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN wasema uko tayari kuongeza misaada kwa Myanmmar

23 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E4se

GENEVA

Mashirika ya misaada pamoja na Umoja wa mataifa yamesema yako tayari kuongeza misaada kwa wahanga wa kimbunga cha Nargis nchini Myanmmar kufuatia tangazo la katibu mkuu Ban Ki Moon kwamba utawala wa kijeshi wa nchi hiyo umekubali kuruhusu wafanyikazi wa misaada kuingia nchini humo.

Hata hivyo maafisa wa Umoja wa mataifa wamesema kwanza wanahitaji kujua maelezo zaidi juu ya uamuzi huo wa serikali ya Myanmmar .Msemaji wa Umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya mashirika ya misaada Elisabeth Byrs amesema mashirika hayo yamekuwa yakikusanya vyakula na mahitaji mengine kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu zaidi ya millioni mbili walioathirika na kimbunga.Utawala wa kijeshi wa Myanmmar umekubali kuruhusu wafanyikazi wa misaada baada ya kufanyika mazungumzo ya kina kati ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon na kiongozi wa kijeshi Than Shwe huko Naypyidaw.