1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaidhinisha mapigano kusitishwa Gaza

Thelma Mwadzaya9 Januari 2009

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kuunga mkono mswada wa azimio linalotoa mwito wa kusitisha moja kwa moja mapigano kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/GUxe
Nembo ya Umoja wa MataifaPicha: AP/DW Fotomontage

Azimio hilo limepitishwa na nchi wanachama 14.Marekani imezuia kura yake.

Mswada wa azimio hilo uliopendekezwa na Uingereza na kuungwa mkono na Marekani na Ufaransa uliweza kupatikana baada ya kufanywa majadiliano marefu na makubaliano kupatikana kati ya wanadiplomasia wa nchi za Kiarabu na za Magharibi.Haijulikani kwa umbali gani Israel na Hamas zitatimiza masharti ya makubaliano hayo.

Miswada mingine iliyopendekezwa hadi hivi sasa kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza ilipingwa na Marekani na Uingereza.