1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNAMID yaongezewa muda zaidi Darfur

Kalyango Siraj1 Agosti 2008

Sudan yaonya dhidi ya Bashir kushtakiwa

https://p.dw.com/p/EoOS
Afisa mmoja wa kijeshi akikagua kikosi cha kulinda amani Darfur cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMIDPicha: AP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limerefusha kwa muda wa mwaka moja kazi za kikosi cha kulinda amani nchini Sudan.

Kwa upande mwingine baraza hilo limekataa madai ya Libya na Afrika Kusini ya kuahirisha harakati za kutolewa waranti wa kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir.

Baada ya kucheleweshwa na malumbano ya kidiplomasia,baraza la wajumbe 15 hatimae limekubali kwa wingi wa kura kutafakari tu kauli ya Umoja wa Afrika kuhusu hatua dhidi ya uwezekano wa kufunguliwa mashtaka rais wa Sudan Hassan al Bashir.

Marekani haikupiga kura.Balozi wake Alejandro Wolf amesema kuwa Marekani inaunga mkono hatua za kuwafikisha mahakamani wale wote waliohusika na makosa katika eneo la Darfur.

Azimio lilitayarishwa na Uingereza na kuweka kifungu ambacho kinagusia kauli ya mataifa ya afrika kuhusu Bashir.Kujiondoa kwa Marekani kungesababisha ombwe la kisheria kwa kikosi hicho.Lakini wajumbe wengine waliobaki 14 wote wakapiga kura ya kuunga azimio hilo bila kupingwa.Hilo walitaka kuonyesha kuunga kwao mkono umuhimu kikosi hicho.

Balozi wa Uingereza kwenye umoja wa Mataifa John Sawers,alieongoza majadiliano kuhusu muswaada huo, amesema kuwa amesikitishwa na kile alichoita kuwa na msiamamo mmoja ,akimaanisha kujiondoa kwa Marekani.

Aidha amelaani kuunganisha suala la mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC na juhudi za kuongeza mda wa kikosi cha kulinda amani kinachoitwa UNAMID kwa kifupi.

Jeshi la UNMID ambalo ni mseto wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika liliundwa mwaka mmoja uliopita na mda wake ulikuwa unamalizika mwezi wa Julai.

Na ingawa jeshi hilo liliundwa mwaka moja uliopita lakini hadi sasa kuna theluthi moja ya askari elf 26 waliopangwa kupelekewa Darfur.

Askari hao wanajeshi pamoja na polisi wana kibarua kigumu cha kukomesha mauaji katika eneo hilo.

Baraza la usalama limekaribisha mipango ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki-moon kuona kama asili mia 80 ya askari hao inatumwa katika neo la Darfur.

Baraza hilo limewahimiza wanachama hatimae kutoa ndege za helikopta 18 zinazohitajika kwa ajili ya kazi hiyo.Umoja wa mataifa unakadiria kuwa mgogoro huo ambo umedumu kwa miaka mitano umesababisha takriban watu laki tatu kupoteza maisha yao ilhali wengine zaidi ya millioni mbili kuachwa bila makazi.

Yeye balozi wa Sudan kwenye Umoja wa Mataifa Abdalmahmoud Abdalhaleem amefurahishwa na kupasishwa kwa azimio hilo na pia pendekezo la kuwa baraza litajadilia kuzuia hatua yoyote ya mahakama ya kimataifa ya mjini the Hague ya ICC dhidi ya rais Bashir. Pia ameonya kuwa hatua yoyote ya kumshataki Bashir itakuwa na madhara makubwa.

Upigaji kura wa azimio hilo uliahirishwa mara kadhaa wajumbe wakijaribu kuishawishi Marekani kuupigia kura ya ndio.