1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wajadili marudio ya uchaguzi Istanbul

Sudi Mnette
7 Mei 2019

Mgombea upinzani ambae ameondolewa katika nafasi yake ya umeya baada ya kutolewa uamuzi tata wa kurejewa kwa uchaguzi wa jiji la Istanbul, Uturuki anafanya mazungumzo na kiongozi wa chama yenye lengo la kujadili mkakati.

https://p.dw.com/p/3I45Q
Türkei, Istanbul: Bürgermeister Ekrem Imamoglu hält Ansprache
Picha: Getty Images/B. Kara

Chama kikuu cha upinzani cha CHP kimelaani uamuzi huo uliotolewa na bodi ya juu kabisa ya uchaguzi wa kurejea uchaguzi kwa kusema "Sio kwa kidemokrasia na wala hauna uhalali". Ekrem Imamoglu, ambaye alishinda katika uchaguzi uliovurugika, amekutana na kiongozi wa chama chake cha CHP, Chifu  Kemal Kilicdoroglu na baadaye atakutana na kiongozi mwingine wa kiitwacho Good Party Meral Aksener.

Mazungumzo hayo yanafanyika siku moja baada baraza la juu kabisa la uchaguzi YSK kutaka kurejewa tena kwa uchaguzi wa jiji la Istanbul, baada ya chama tawala cha rais Recep Tayyip Erdogan kulalamika kuhusu kile ilichokiita ukiukwaji na kuwepo kwa vitendo vya uhalifu wa kupangwa.

Istanbul kiini cha mzozo

Türkei, Istanbul: Bürgermeister Ekrem Imamoglu hält Ansprache
Wafuwasi wa mwanasiasa wa upinzani Ekrem ImamogluPicha: Getty Images/AFP/B. Kilic

Kushindwa kwa chama cha Haki na Maendeleo AKP, katika jiji la Istanbul, likiwa kama kitovu cha uchumi na jiji kubwa nchini Uturuki kumekuwa jambo la kustusha sana kwa chama hicho. Chama hicho na watangulizi wake kilimelitawala jiji hilo klwa takribani miaka 25. Imamoglu, meya wa zamani, alitoa matumaini kwa upande wa upinzani baada ya ushindi wake wa kushangaza katika jiji hilo la Istanbul.

Ushindi wake mwembamba, ulikuwa una salamu muhimu kwa Erdogan, ambaye amekulia katika jiji hilo na kuendeleza nguvu zake za kimamlaka kama waziri mkuu na baadaye kuhudumu katika nafasi ya urais ambapo pia aliwahi kuwa meya. Katika hotuba yake Imamoglu amejigamba kuwa hatorejea nyuma, zaidi ataibuka na ushindi mnono katika uchaguzi mpya wa jiji hilo uliopangwa kufanyika Juni 23."Ninatoa wito kwa wale ambao walifanya uamuzi huo wa ulaghai katika baraza Kuu la Uchaguzi Kuu. Mniamini, nitaokoa hata maisha ya watoto wao na wajukuu kupitia ujumbe huu ninaoutoa hapa." alisema  Imamoglu.

Akizungumza na maelfu ya wafuasi wake katika wilaya ya Beylkduzu, katika viunga vya jiji la Istanbul, eneo ambalo aliwahi kuwa meya alisema "Unaweza ukawa umegadhibishwa lakini kamwe usipoteze tumaini lako," maelfu ya wafuawasi wa Imamoglu waliingia mitaani katika wilaya ya Kadikoy mjini Istanbul, eneo ambalo litajwa kama ngome ya CHP kupinga kurejewa kwa uchaguzi wa jiji hilo.