Urithi uliopitwa na wakati: Ujamaa barani Afrika
Uhusiano wa Afrika na nchi za ujamaa ni mada kuu katika maonesho ya Iwalewahaus, Bayreuth, ambapo maudhui ya ''Things Fall Apart'' yanaangalia hali ya sasa na enzi za Usovieti kuhusu mtangano kambi ya Mashariki.
Mashubaka makongwe, muonekano mpya
Wakati nchi za Kiafrika zikiwa zimeshajikomboa kutoka kwa wakoloni wao mwishoni mwa miaka ya 1950,nchi nyingi za wakoloni ziliingia katika vita vya nadharia vilivyolitumbukiza pia bara la Afrika katika vita baridi: Kauli mbiu kama Afrika inapambana - Afrika inashinda'' Umoja wa Sovieti ulijipatia umaarufu katika nchi changa za Afrika.
Utopia yaota kutu
Mapenzi ya Udugu kati ya nchi za Umoja wa Sovieti na Afrika yalidumu kwa miongo michache tu. Lakini imeacha alama hadi wakati huu. Mpiga picha wa Angola Kilonji Kia Henda mwaka 2006 aligundua Meli moja ya makaburi iliyochora Karl Marx kaskazini mwa Luanda. Ilikuwa sehemu ya meli za uvuvi zilizopewa Angola na Umoja wa Sovieti kama msaada, na zilitumiwa kwa miaka michache tu.
Vita vya mamluki Afrika
Historia ya Ujamaa Angola inajitokeza kupitia picha za ukutani za kina Leonid Brechnew, Fidel Castro na katikati ni Agostinho Neto rais wa kwanza wa Angola ambazo zilipigwa na mpiga picha wa Afrika Kusini Jo Ractliffe. Katika vita vya Angola Cuba ilituma wanajeshi,Umoja wa Sovieti ilimpelekea silaha Neto.Na upinzani ulikuwa ukipata msaada wa fedha na silaha kutoka Afrika Kusini na Marekani.
Kumbukumbu kwa mpinzani wa ubeberu
Hata Patrice Lumumba waziri mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliunga mkono Ujamaa. Katika mgogoro ulioikumba serikali changa ya taifa hili aliomba msaada wa Umoja wa Sovieti. Na kutokana na hilo alipingwa na baadae chini ya uangalizi wa majaasusi wa Ubelgiji aliuwawa. Shujaa huyu wa vita vya ukombozi wa Afrika anaenziwa kwa kuwepo stampu za barua za picha yake.
Munaalikwa lakini sio kukaribishwa
Urusi iliwachukua wanafunzi wengi kutoka Kongo. Waliosomea katika chuo kikuu cha Patrice Lumumba katika mji mkuu wengi walipata ufadhili wa kwenda kusomea nadharia. Wengi, hata hivyo, mara nyingi walikuwa wakibaguliwa na waliandamana. Maandamano ya mwisho ya hadharani ya wanafunzi wa Kiafrika yalishuhudiwa mwishoni mwa miaka ya 1950 baada ya utawala wa Stalin.
Brezhnev: Matumizi ya ardhi ya Afrika
Umoja wa Sovieti haukutumia gharama wala juhudi kuendeleza nadharia yake katika Afrika. Ziara ya Leonid Brezhnev nchini Guinea mwaka 1957 ilitengenezwa filamu. Alexander Markov alikuja baadae kutengeneza filamu iliyofuatilia propaganda hiyo. Mwaka 2015 filamu hiyo ilichaguliwa katika maonesho ya filamu ya mjini Berlin, Berlinale.
Kuungana kwenye eneo moja
Ilikuwa rahisi kueneza propaganda kwa njia ya sauti na picha. Kwa kuoneshwa picha za watoto kutoka mabara matatu hiyo ilikuwa njia iliyotowa mafanikio makubwa katika kuwafikia watu. Kwa watoto wengi hiki ni kitu kilichowatia nguvu. Kuwapa matumaini ya kuweza kushiriki kwa pamoja katika safari ya kuuona ulimwengu.
Kuushangiria Ujamaa
Ethiopia kama makao makuu ya Umoja wa Afrika ilikuwa kama ufunguo wa Afrika. Utawala wa kijeshi chini ya Mengistu Haillemariam ulikuwa na mengi ya kuushukuru Umoja wa Kisovieti. Wageni wote wa makao OAU walikaribishwa na mtawala aliyekuwa na nguvu Lenin. Sanamu la Marx lililoenziwa Erich Honecker katika mwaka wa 10 wa Jubilee ya Mapinduzi bado ipo katika bustani ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa.
Uhalali wa zama za Kisoshalisti
Hadi wakati huu watawala wa Afrika wanakasumba za Ujamaa. Sanamu hili la shaba linalobeba kauli mbiu ya Afrika imezaliwa upya, imejengwa mwaka 2010 na Rais wa Senegal Abdoulaye Wade. Ilibuniwa na kutengenezwa na kampuni ya Korea Kaskazini ambayo imehusika na ujenzi mjini Addis Ababa na katika nchi miji mingine 20 barani Afrika.
Sanaa ya ukweli wa kisoshalisti
Mwaka 2005, Rais wa Botswana Festus Mogae alizindua kuwekwa kwa picha za viongozi wakuu watatu. Waanzilishi wa taifa hilo. Mkorea Kusini Onejoon Che anaonesha picha hizo ambazo ni kiashirio cha uhalisia wa kasumba za ujamaa barani Afrika ambao hadi wakati huu unaungwa mkono na watawala wengi wa Kiafrika.
Kinachosalia baada ya maonesho
Burkina Faso nchi ya mwisho kujaribu kuanzisha ujamaa barani Afrika. Ougadougou mji mkuu wa maonesho ya Filamu za Kiafrika zinaoneshwa pia filamu kama zile zinazosimulia mtu kama Ousmane Sembene binafsi alivyosomea Moscow. Mfuasi mkubwa wa Ujamaa Thomas Sankara alikuwa mtu muhimu aliyeunga mkono maonesho ya Fespaco. Picha zilizochukuliwa 2005 na Issac Julien zimeonesha kumbi zikiwa tupu.
Karibuni kwenda Afrika?
Katika maonesho ya ''Things fall apart'' mjini London na Bayreuth ambayo yanaendelea hadi Jumapili (18.09.2016). Kuanzia mwezi Desemba kwa miezi miwili mjini yatakuwa Budapest. makumbusho ya Iwalewahaus mjini Bayreuth yako katika mazungumzo na taasisi ya Goethe kuhusu kuyapeleka maonesho hayo Afrika. Ndoto ya ujamaa barani Afrika pia bado imebakia kuwa hadithi.