1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na NATO, hazijaafikiana juu ya Libya

Halima Nyanza (ZPR)5 Julai 2011

Mkutano kati ya Urusi na Jumuia ya Kujihami ya NATO umemalizika kwa pande zote mbili kutoafikiana juu ya operesheni za kijeshi zinazofanywa nchini Libya.

https://p.dw.com/p/11ovp
Rais wa Urusi Dmitry Medvedev (kulia) na Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh RasmussenPicha: picture-alliance/dpa

Katika mkutano huo uliofanyika katika mji wa Sochi nchini Urusi, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi Sergei Lavrov ameituhumu NATO kwa kwenda mbele zaidi katika kulitafsiri azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Libya.

NATO Russland Sotschi
Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei LavrovPicha: picture-alliance/dpa

Urusi imeukosoa hasa uamuzi wa Ufaransa kuwapatia silaha waasi wa Libya.

Lakini hata hivyo Katibu mkuu wa jumuia hiyo ya NATO, Anders Fogh Rasmussen ametetea hatua hiyo kwa kusema kuwa itahitajika kwa ajili ya kuwalinda raia kutokana na mashambulio yanayofanywa na majeshi ya Libya yanayoongozwa na kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.

Royal Air Force Typhoon
Ndege za kijeshi za NATOPicha: picture alliance/dpa

Aidha ametetea pia mpango wa jumuia hiyo wa kuunda mfumo wa kinga dhidi ya makombora barani Ulaya, ambao Urusi inaona ni kitisho kwa usalama wake.