1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WADA yaja juu kuhusu doping

16 Novemba 2015

Shirika la dunia la kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu misuli, Doping, WADA linatarajiwa kutoa uamuzi dhidi ya shirika la kupambana na Doping la Urusi

https://p.dw.com/p/1H6mG
WADA empfehlt Russland Ausschluss Symbolbild Station für Dopingkontrolle in Sotschi
Picha: picture alliance/epa/H. Schmidt

Uamuzi huo utatolewa katika mkutano muhimu mjini Colorado nchini Marekani siku ya Jumatano ambao utalenga kuweka mikakati kwa ajili ya vita dhidi ya Doping duniani.

Uongozi wa WADA utakutana kutathmini uchunguzi wao wa jopo lake huru , ambalo limefichua mpango mkubwa uliokuwa ukiungwa mkono na taifa wa Doping nchini Urusi ambao umeutumbukiza mchezo wa riadha katika mzozo mkubwa katika historia.

Shirika la vyama vya riadha duniani IAAF siku ya Ijumaa limewazuwia wanariadha wa Urusi kushiriki mashindano ya kimataifa, na kuweka ushiriki wa wanariadha hao katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro katika mashaka .

Lakini pia shirikisho la kimataifa la vyama vya riadha IAAF linaweza kukabiliana na uwezekano ambao ni pamoja na kuondolewa kutoka katika mashindano ya Olimpiki wakati sehemu ya pili ya shirika la kupambana na Doping itakapowasilishwa, kwa mujibu wa mmoja wa makamishina wa tume huru ya shirikisho hilo. Lakini uamuzi wowote wa kuisimamisha IAAF kutoshiriki katika michezo utahitaji kufanywa na kamati maalum ya kimataifa ya Olimpiki IOC.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman