1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatafuta muujiza, Messi na Ronaldo nje

Sekione Kitojo
1 Julai 2018

Urusi yatumai  kufanya maajabu fainali  za kombe la dunia leo wakati  mwenyeji hao wakijitayarisha kutiana kifuani na mabingwa  wa mwaka 2010 Uhispania wakiwania  nafasi  katika  robo fainali.

https://p.dw.com/p/30cIz
FIFA Fußball-WM 2018 | Achtelfinale | Uruguay vs. Portugal | JUBEL Uruguay
Picha: Reuters/T. Hanai

Wakati  wenyeji  Urusi wakijitayarisha  kuvaana  na  Uhisoania , Cristiano Ronaldo na  Lionel Messi wameyaaga  mashindano.

Michezo mingine  ya  kundi  la  timu  16 zilizobakia  katika  fainali  hizi zinawakutanisha  timu  ya  Croatia  yenye  wachezaji  wenye vipaji wakiongozwa  na  Luka  Modric, timu  ambayo  ina  rekodi  safi  katika  awamu ya  makundi ikicheza  dhidi  ya  Denmark, lakini watahitaji kupata uchawi uliofanyika  katika kasheshe iliyotokea  katika  michezo  ya  kwanza  ya awamu  hii  ya  mtoano jana  Jumamosi.

FIFA Fußball-WM 2018 | Achtelfinale | Frankreich vs. Argentinien | 3. TOR Frankreich
Kylian Mbappe akishangiria bao lake dhidi ya ArgentinaPicha: Reuters/M. Dalder

Ufaransa iliipiga mweleka  Argentina kwa  mabao 4-3  katika  pambano  kali la  kombe  la  dunia, wakati  kijana  wa  miaka  19 Kylian Mbappe alijitangaza katika  medani  hii  kubwa  ya  dunia kwa  kupachika  ambao  mawili  na  Le Bleus  waliwarejesa  nyumbani makamu bingwa  wa  dunia  wa  mwaka  2014.

Mbappe  alikuwa  kijana  wa  kwanza  kufunga  mabao  mawili  katika  fainali za  kombe  la  dunia tangu  pale  Pele  akiwa  na  umri  wa  miaka  17 alipofunga  katika  fainali  za  mwaka  1958.

Mchezaji  huyo  mkongwe  wa  Brazil  aliandika  katika  ukurasa  wa  Twitter akimzungumzia Mfaransa  huyo: "Hongera  kwa  Mbappe, mabao 2  katika kombe  la  dunia  kwa  kijana  mdogo  namna  hiyo yanakuweka  katika kundi la wakubwa."

FIFA Fußball-WM 2018 | Achtelfinale | Frankreich vs. Argentinien | 3. TOR Frankreich
Kylian Mbappe tena akipachika bao la nne kwa UfaransaPicha: Reuters/P. Olivares

Messi  na  Ronaldo washindwa kufunga katika  awamu ya  mtoano

Messi  hata  hivyo  alishindwa  kufumania  nyavu, akiondoka  nchini  Urusi akiwa  na  bao 1, na  mchezaji  huyo  mwenye  umri  wa  miaka  31 anayechezea  klabu  ya  Barcelona huenda  amekwisha  tanabahi  kuwa hakuna  tena  nafasi  ya  kushinda  kombe  la  dunia.

Baadaye  mjini  Sochi, Ronaldo, ambaye  alianza  kombe  la  dunia  kwa kufunga  mabao 3 dhidi  ya  Uhispania, hakuna  na  uwezo tena  kuizuwia Ureno  kuteleza  nje  ya  mashindano  hayo  wakati Edinson Cavani alipotundika  mpira  mara mbili  wavuni   katika  ushindi  wa  mabao 2-1 na kuwarejesha  mabingwa  hao  wa  bara  la Ulaya  nyumbani.

FIFA Fußball-WM 2018 | Achtelfinale | Frankreich vs. Argentinien | 2. TOR Argentinien
Hata hivyo furaha ya Argentina haikufika mbali, Lionel Messi akifurahia bao la ArgentinaPicha: Reuters/C.G. Rawlins

Cavani , ambaye huchezea  timu  moja  na  Mbappe  katika  klabu  ya  Paris Saint-Germain, alifungua  kitabu  cha  mabao  akiruka  juu na  kuuweka  mpira wavuni  kabla  ya  kufunga  kwa ustadi  mkubwa akimwacha  mlinda  mlango Rui Patricio  akishindwa  kufanya  lolote  kuzuwia  mkwaju  huo na  kuwa   bao la  ushindi  katika  mchezo  huo baada  ya  Pepe  kusawazisha  hapo  kabla.

Licha  ya  kwamba  mchezaji  huyo  wa  Uruguay  alichechea  wakati  akitoka uwanjani  kwa  maumivu , baadaye  alisema aligongwa  tu  na  anatarajia kurejea  uwanjani  kupambana  na  ufaransa   katika  robo  fainali.

FIFA Fußball-WM 2018 | Achtelfinale | Uruguay vs. Portugal | Enttäuschung Ronaldo
Ronaldo CR7 kichwa chini akitoka uwanja bila mafnikio dhidi ya UruguayPicha: Reuters/J. Silva

Ronaldo atakuwa  na  umri  wa  miaka  37 wakati  fainali  nyingine  za  kombe la  dunia  zitakapofanyika  nchini  Qatar, lakini  hakutaka  kuingizwa  katika mjadala  iwapo  anapanga  kuachia  ngazi  katika  timu  ya  taifa.

"Huu  si  wakati  wa  kuzungumzia juu  ya  hatima  yangu na  makocha," alisema  Ronaldo, ambae, kama  Messi , anaondoka  katika  fainali  za kombe  la  dunia akiwa  hajafunga  bao  katika  awamu  ya  mtoano.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / rtre

Mhariri:  Zainab Aziz