1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama wa vinu vya nyuklia Japan

15 Machi 2011

Viwango vya miale ya nyuklia vimezidi kufuatia mripuko mwingine uliotokea hii leo (Jumanne) katika kinu cha Fukushima Daiichi.

https://p.dw.com/p/10Z9A
Vikosi vya jeshi vimejihami kwa mavazi ya kujikinga na sumu ya nyuklia huku wakiendelea na jitihada za uokowaji.Picha: picture-alliance/dpa

Waziri mkuu wa Japan, Naoto Kan, hii leo amesema kuwa viwango vya miale ya sumu yamezidi katika kinu cha nyulia kilicho athirika na tetemeko la ardhi, baada ya kutokea mripuko mwingine hii leo, na kuwa kuna hatari ya sumu hiyo kuvuja na kuingia hewani.

Premierminister Japan Naoto Kan zum Erdbeben
Waziri mkuu wa Japan, Naoto Kan.Picha: AP

Waziri mkuu Kan amewaomba watu walio umbali wa kilomita 30 kutoka kinu hicho kilichopo kaskazini mwa mji mkuu Tokyo, wajifungie ndani. Ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu huo, umeonya katika tahadhari yake, kuwa viwango vidogo vya upepo wa miale hiyo ya sumu, huenda vikafika mjini Tokyo katika muda wa masaa 10. Mripuko wa hivi leo ni wa tatu katika kinu hicho tangu kuathirika na tetemeko la ardhi na tsunami siku ya Ijumaa. Maafisa wa serikali wamekuwa wakijaribu kuzuiwa kuyeyuka mafuta kwenye vinu hivyo vitatu vya Fukushima Daiichi kwa kuvimwagia maji ya baharini ili kuvipoesha.

Japan Fukushima Erdbeben AKW Block 3
Picha: Kyodo News/AP/dapd

Huku kukiwa na wasiwasi kuhusu athari ya kuanguka uchumi kutokana na majanga hayo mawili, hisa za Japan zilishuka kwa asilimia 7.0, hadi viwango vyake vya chini ambavyo havijashuhudiwa kwa kiasi ya miaka 2.

Hasara kamili ya majanga hayo bado inabainika, huku waokowaji wakiendelea na shughuli hizo za uokozi katika eneo la kaskazini, ambapo maafisa wa serikali wanasema kiasi ya watu 10,000 waliuwawa.

Mwandishi:Maryam Abdalla/Rtre/Dpae/Afpe

Mhariri:Hamidou Oummilkheir