1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama waimarishwa katika Ruhr derby

25 Machi 2014

Jukwaa liko tayari kwa mchuano mkali katika soka la Ujerumani, wa watani wa jadi Borussia Dortmund na Schalke. Mpambano huo unaweza kuamua ni nani atakayemaliza katika nafasi ya pili msimu huu.

https://p.dw.com/p/1BVLc
Dortmund Schalke Fankrawalle Derby Ausschreitungen 20.10.2012
Picha: picture-alliance/dpa

Joto limepanda kwa kivumbi hicho katika uwanja wa Dortmund, Westfalenstadion, ambapo Schalke wako nyuma ya mahasimu BVB na tofauti ya point moja. Shirikisho la Soka Ujerumani - DFB limetoa onyo la mwisho kwa Borussia Dortmund kuwadhibiti mashabiki wao huku polisi wakitarajia kutokea vurugu za mashabiki katika pambano hilo ..

Karibu mashabiki 200 walikamatwa baada ya kutokea makabiliano wakati Dortmund ilipokuwa mwenyeji wa mchuano huo mwezi Oktoba 2012 na kukawa na vurugu kabla ya mchuano wa Oktoba mwaka jana nyumbani kwa Schalke 04, Gelsenkirchen.

Takribani polisi 3,000 wanatarajiwa kuwa zamuni leo katika mojawapo ya operesheni kubwa zaidi za polisi katika mchuano wa soka nchini Ujerumani.

Siku ya mchezo ilisongezwa hadi saa mbili usiku saa za Ujerumani na polisi wanasema karibu mashabiki 500 wenye kusababisha vurugu kutoka timu zote mbili na watu wengine 90 tayari wamepigwa marufuku.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Abdulrahman