1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushirikiano wa kibiashara ya Ujerumani na Urusi

Saumu Ramadhani Yusuf11 Oktoba 2010

Rais wa Ujerumani ziarani Moscow

https://p.dw.com/p/PbUI
Rais wa Ujrumani Christian WulffPicha: picture alliance/dpa

Rais wa Ujerumani Christian Wulff anaelekea Urusi hii leo kwa ziara ya siku tano yenye lengo la kutafuta ushirikiano zaidi wa kiuchumi pamoja na kisiasa na taifa hilo.Ziara hiyo ni ya kwanza tangu mwaka 2002 kuwahi kufanywa na kiongozi wa serikali wa Ujerumani nchini Urusi.

Ziara ya rais Christian Wulff nchini Urussi ilipangwa miezi kadhaa iliyopita na mtangulizi wake Horst Koehler kabla ya kjiuzulu kwake madarakani mnamo mwezi Mei.Katika ziara hiyo rais wa Ujerumani atatembelea pia mji wa Twer ambao unaushirikiano  na mji wa Osnabrueck nchini Ujerumani,na baada ya hapo ataelekea St Petersburg.rais Wulff pamoja na mkewe Bettina wakiwa Urussi pia watapanda treni mpya ya mwendo wa kasi inayofahamika kama Sapsan iliyoundwa na kampuni la Siemenes la Ujerumani.

Dmitry Medvedev und Angela Merkel Flash-Galerie
Rais Dmitry Medvedev na Kansela Angela Merkel katika mazungumzo ya kibiashara mwezi JulyPicha: Picture alliance/dpa

Treni hizo za Sapsan ndio treni za mwendo wa kabisa kabisa nchini Urussi na zimekuwa mara nyingi zikishambuliwa na wakaazi walio na hasira wanaopinga kile wanachosema kuondolewa kwa treni za bei nafuu.Katika kipindi cha wiki kadhaa vyombo vya habari nchini Urussi vimekuwa vikijadili  athari za technologia hiyo ya kisasa katika taifa hilo  ambalo bado linaangaliwa kama taifa maskini lenye ambalo mikoa yake mingi bado iko nyuma kimaendeleo tangu utawala wa sovieti.

Itakumbukwa kwamba wakati wa ziara ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel nchini humo mwezi July rais Dmitry Medvedev aliipa nafasi ya kwanza Ujerumani  katika kuleta maendeleo ya kisasa nchini Urussi  na bila shaka hilo ni jambo ambalo linatarajiwa kuendelezwa na rais Wulff.Rais huyo anatazamiwa kukutana na Medvedev  mjini Moscow na pia amepangiwa kukutana na waziri mkuu Vladmir Putin.Aidha amepangiwa kukutana na kiongozi wa madhehebu ya Othodox nchini humo pamoja na vyama vya kiaraia.Inatarajia kwamba rais Wulf pia atatoa shukurani zake kuhusiana na jukumu la Umoja wa Sovieti  katika kufanikisha hatua ya kumaliza vita baridi  pamoja na  juhudi za nchi hiyo zilizochangia kumaliza utawala wa Hitler nchini Ujerumani.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo nchi Urussi kama vile  Vladislav Belov wanasema kwamba ziara hiyo ya rais wa Ujerumani haiwezi kuwa na matokeo ya maana hasa ukizingatia madaraka ya kiongozi huyo.Vladislav Belov anasema warussi wengi hawafahamu jukumu la rais wa Ujerumani ambaye ana madaraka machache  ukilinganisha na madaraka ya rais wa Urusi.Rais Wulff ambaye anaandamana na ujumbe wa wanauchumianatazamiwa kulenga zaidi katika masuala ya kiuchumi huku akipangiwa pia kutoka hotuba  yake kwa wanafunzi wa masuala ya biashara mjini Moscow pamoja na kuhudhuria  maonesho ya kiuchumi katika mji wa Uljanovsk ulioko kilomita 700 mashariki ya mji wa Moscow.

Mwandishi Saumu Mwasimba/DPAE

Mhariri :M.AbdulRahman